Skip to main content

SHAIRI MAISHA MAZURI NI YA MJINI AU VIJIJINI?

MAISHA MAZURI NI YA MJINI AU VIJIJINI?

Uledi nilitembea, mjini na vijijini
Ndipo nilipogundua, maisha mema mjini
Nakupa zangu hisia, na mawazo akilini

vijini ni sulubu, kazi bila maakuli
Duka halipo karibu, kilimo na jua kali
Maishaye ni adhabu, wakazi hawana hali

Pole kwa safari yako, mijini na vijijini
Nami nilikuwa huko, nimechunguza makini
vijijini mahangaiko, vukumbo na urubini

Kule ardhi ni tele, tunajenga kwa nafasi
Tunajijengea shule, wakazi sisi kwa sisi
Mambo yasonga mbele, kwa mapigo si matusi

Mjini njia za lami, viijijini vumbivumbi
Mabasi ni kwa makumi, vijijini hawatambwi
Mjiji mimi sihami, hapa nimejenga kambi

Rafiki yangu miminaona, manufaa kotekote
Kote kwasaidiana, vijiji vina matete
Si vizuri kuvutana, ili nikuzidi kete

Miji na vijiji ndugu, mapacha kwa kuzaliwa
Ndugu tusifanye shari, sote tutembeleane
Miji na vijiji shwari, bidhaa tuuziane

Wewe na mimi kufu, kwa mawazo mwanana
Haifai kukashifu, kashifa si mwanana

Comments