Matini hii ya
Mofolojia ya Kiswahili sanifu kwa sekondari na vyuo inachukua nafasi yake
katika Mofolojia ya Kiswahili ambacho bado haijachapishwa kuwa kitabu rasmi
kipo katika marekebisho kuanzia mwaka 2017.
Kwa hakika
matini hii ni moja ya matini ambayo huweza kukidhi mahtaji ya kufundishia somo
la Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Matini hii
imetayarishwa katika muktadha wa kukidhi Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu.
Matini hii ni tofauti
na mtini nyingine za awali kwa namna kadhaa. Kwanza matini hii imeelezea fasili
ya mofolojia kama taaluma nyingine za isimu ya lugha katika Kiswahili. Pili
dhana kadha wa kadha ambazo zilikuwa zinachanganya au zina maelezo pungufu
katika matini za awali zimetazamwa upya na kupewa maelezo ya kina na uwazi
zaidi hasa dhana ya mofu na mofimu zinavyochanganywa na wataalamu mbalimbali.
Pia hali hii inajidhirisha katika alomofu, dhana ya mofofonolojia, unyambuaji,
uambishaji na uundaji wa maneno. Dhana ya sarufi maumbo ambayo ndiyo kiini cha
matini hii imepewa maelezo kamilifu zaidi kuliko ilivyoelezwa na wanaisimu wa
mwanzoni
Kwa ujumla
naweza kusema kuwa matini hii imeandaliwa kukidhi kwa kuzingatia kumlenga zaidi
mwanafunzi wa sekondari kuliko kulenga uwanja mwenyewe wa mofolojia. Kutokana
na hali hii ni matumaini yangukwamba wanafunzi watanufaika sana na matini hii.
Lakini yaffa nikumbushie hapa kwamba mwanafunzi atanufaika zaidi iwapo atatumia
matini hii sambamana Mofolojia ya Kiswahili.
Comments
Post a Comment