. DUNIA MTI MKAVU
Hekima na busara ni sawa na ujinga na upumbavu
Furaha na kicheko ni sawa na huzuni na kilio
Sehemu yenye mwanga ni sawa na sehemu yenye giza
Ukitenda wema unaweza kulipizwa kwa mateke
Ukitenda mabaya unaweza kulipizwa kwa wema
Binadamu anamdharau panzi kwa sababu ni mdudu
Lakini tambueni panzi atakuja kuwa na thamani kama ng'ombe

Mwenzako akimwaga ugali mwaga unga
Na mwenzako akimwaga mboga mwaga mafuta
Mwanadamu kama hujui ndoa ni mkono karibu na goli
Na firimbi imelia golini hamna mtu
Lakini goli upana futi moja viatu vimechanika na mpira ni tofari
Uwanja kijiji ndani ya nyumba
Washangiliaji na wazomeaji wengi sana
Maswali mengi kama hayo manung'uniko mengi kama hayo
Matatizo mengi kama hayo sasa
Yanaonekana ingawa zamani hayakuwako
Lakini haya yote yataisha
Binadamu wenzangu tambueni dunia hii imegeuka.
Kushoto kumekuwa kulia na kulia kumekuwa kushoto
Dunia imegeuka kuwa tambala bovu
Kazi nzuri mno
ReplyDeletekeep it up kazi nzur
ReplyDeletekazi nzuri sana hongera
ReplyDeleteKazi nzurii ila nilihitaji kujua uhusiano uliopo kati ya Mofu na mofimu
ReplyDeleteKazi safi sana!
ReplyDeleteNimeipenda sanaa