Skip to main content

SHAIRI DUNIA MTI MKAVU

.                           DUNIA MTI MKAVU
Hekima na busara ni sawa na ujinga na upumbavu
Furaha na kicheko ni sawa na huzuni na kilio
Sehemu yenye mwanga ni sawa na sehemu yenye giza
Ukitenda wema unaweza kulipizwa kwa mateke
Ukitenda mabaya unaweza kulipizwa kwa wema
Binadamu anamdharau panzi kwa sababu ni mdudu
Lakini tambueni panzi atakuja kuwa na thamani kama ng'ombe

Mwenzako akimwaga ugali mwaga unga
Na mwenzako akimwaga mboga mwaga mafuta
Mwanadamu kama hujui ndoa ni mkono karibu na goli
Na firimbi imelia golini hamna mtu
Lakini goli upana futi moja viatu vimechanika na mpira ni tofari

Uwanja kijiji ndani ya nyumba
Washangiliaji na wazomeaji wengi sana
Maswali mengi kama hayo manung'uniko mengi kama hayo
Matatizo mengi kama hayo sasa
Yanaonekana ingawa zamani hayakuwako
Lakini haya yote yataisha
Binadamu wenzangu tambueni dunia hii imegeuka.
Kushoto kumekuwa kulia na kulia kumekuwa kushoto
Dunia imegeuka kuwa tambala bovu

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

DHANA YA MOFU MOFIMU, ALOMOFU NA MAKUNDI YA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

                                        DHANA YA MOFU, MOFIMU NA ALOMOFU Dhana ya mofu Mgullu, (1999) anasema kuwa dhana za mofu, alomofimu na mofimu ndizo ambazo hutumiwa sana kwa uchambuzi wa kiisimu hususani katika kiwango cha mofolojia. Istilah hizi zote zimetoholewa kutoka istilahi za kingereza, yaani a.       Mofu kutoka morph. b.       Alomofu kutoka allomorph . c.        Mofimu kutoka morpheme Inafaa dhana hizi tatu zielezwe vizuri kwa sababu ni dhana muhimu sana katika isimu. Lakini kwa bahati mbaya dhana hizi huchanganywa changanywa sana wakati wa kuzitumia kiasi ambacho kimefanya dhana hizi zionekane kuwa niza kutatanisha siyo katika uchambuzi wa lugha ya Kiswahili tu bali pia hata lugha ya kiingereza ambako zimetokea. Tunasisitiza hapa kuwa dhana hizi zinafaa zielezwe kwa makini na kw...

Kitabu : Mofolojia ya kiswahili

Matini hii ya Mofolojia ya Kiswahili sanifu kwa sekondari na vyuo inachukua nafasi yake katika Mofolojia ya Kiswahili ambacho bado haijachapishwa kuwa kitabu rasmi kipo katika marekebisho kuanzia mwaka 2017. Kwa hakika matini hii ni moja ya matini ambayo huweza kukidhi mahtaji ya kufundishia somo la Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Matini hii imetayarishwa katika muktadha wa kukidhi Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Matini hii ni tofauti na mtini nyingine za awali kwa namna kadhaa. Kwanza matini hii imeelezea fasili ya mofolojia kama taaluma nyingine za isimu ya lugha katika Kiswahili. Pili dhana kadha wa kadha ambazo zilikuwa zinachanganya au zina maelezo pungufu katika matini za awali zimetazamwa upya na kupewa maelezo ya kina na uwazi zaidi hasa dhana ya mofu na mofimu zinavyochanganywa na wataalamu mbalimbali. Pia hali hii inajidhirisha katika alomofu, dhana ya mofofonolojia, unyambuaji, uambishaji na uundaji wa maneno. Dhana ya sarufi maumbo amba...