TATIZO
Inaonekana kama kwamba
Nje kuna giza lenye mwanga
Na ndani kuna mwanga wenye giza
Nami nimekaa pasi mwanga wala giza
Ni kama noana kama sioni
Nimeinama kichwa karibu kama mjinga
Karibu kama mwerevu. Kusoma siwezi
Kuandika siwezi. Nimeshindwa kujua
Ninachojua. Lakini kitu hiki ni kama
Nakiogopa kama sikiogopi
Inaonekana kama kwamba
Nje kuna giza lenye mwanga
Na ndani kuna mwanga wenye giza
Nami nimekaa pasi mwanga wala giza
Ni kama noana kama sioni
Nimeinama kichwa karibu kama mjinga
Karibu kama mwerevu. Kusoma siwezi
Kuandika siwezi. Nimeshindwa kujua
Ninachojua. Lakini kitu hiki ni kama
Nakiogopa kama sikiogopi
Comments
Post a Comment