Skip to main content

SHAIRI Wahenga Wenye Hekima

                      Wahenga Wenye Hekima


Wahenga husema ulio juu huendeshwa na ulio ndani.
Ukituma watoto wadogo shambani mavuno yatakuwa ya kitoto.
Ukishindwa kurudi na kware rudi na bundi.
Ila kumbuka sisimizi hukusanyika sehemu yenye mfupa.
Ila ndege mwoga ndiye huwa na makinda wengi .
Ndama huzaliwa na masikio na pembe huota baadaye
Mwewe hushinda angani lakini jion ikifika hulazimika kutua porini.
Wengine husema mvua inapotokea kibandani haina pa kukimbilia ila ipo siku msitu Utakuwa na masikio.
Mlima usiosikia huungua watu wakiutazama. leo ngoja nifike kwa wahenga ili tuweze kujadili ila kila ngoma ina mwisho wake

Comments

Popular posts from this blog

DHANA YA MOFU MOFIMU, ALOMOFU NA MAKUNDI YA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

                                        DHANA YA MOFU, MOFIMU NA ALOMOFU Dhana ya mofu Mgullu, (1999) anasema kuwa dhana za mofu, alomofimu na mofimu ndizo ambazo hutumiwa sana kwa uchambuzi wa kiisimu hususani katika kiwango cha mofolojia. Istilah hizi zote zimetoholewa kutoka istilahi za kingereza, yaani a.       Mofu kutoka morph. b.       Alomofu kutoka allomorph . c.        Mofimu kutoka morpheme Inafaa dhana hizi tatu zielezwe vizuri kwa sababu ni dhana muhimu sana katika isimu. Lakini kwa bahati mbaya dhana hizi huchanganywa changanywa sana wakati wa kuzitumia kiasi ambacho kimefanya dhana hizi zionekane kuwa niza kutatanisha siyo katika uchambuzi wa lugha ya Kiswahili tu bali pia hata lugha ya kiingereza ambako zimetokea. Tunasisitiza hapa kuwa dhana hizi zinafaa zielezwe kwa makini na kw...

Kitabu : Mofolojia ya kiswahili

Matini hii ya Mofolojia ya Kiswahili sanifu kwa sekondari na vyuo inachukua nafasi yake katika Mofolojia ya Kiswahili ambacho bado haijachapishwa kuwa kitabu rasmi kipo katika marekebisho kuanzia mwaka 2017. Kwa hakika matini hii ni moja ya matini ambayo huweza kukidhi mahtaji ya kufundishia somo la Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Matini hii imetayarishwa katika muktadha wa kukidhi Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Matini hii ni tofauti na mtini nyingine za awali kwa namna kadhaa. Kwanza matini hii imeelezea fasili ya mofolojia kama taaluma nyingine za isimu ya lugha katika Kiswahili. Pili dhana kadha wa kadha ambazo zilikuwa zinachanganya au zina maelezo pungufu katika matini za awali zimetazamwa upya na kupewa maelezo ya kina na uwazi zaidi hasa dhana ya mofu na mofimu zinavyochanganywa na wataalamu mbalimbali. Pia hali hii inajidhirisha katika alomofu, dhana ya mofofonolojia, unyambuaji, uambishaji na uundaji wa maneno. Dhana ya sarufi maumbo amba...

SHAIRI DUNIA MTI MKAVU

.                           DUNIA MTI MKAVU Hekima na busara ni sawa na ujinga na upumbavu Furaha na kicheko ni sawa na huzuni na kilio Sehemu yenye mwanga ni s awa na sehemu yenye giza Ukitenda wema unaweza kulipizwa kwa mateke Ukitenda mabaya unaweza kulipizwa kwa wema Binadamu anamdharau panzi kwa sababu ni mdudu Lakini tambueni panzi atakuja kuwa na thamani kama ng'ombe Mwenzako akimwaga ugali mwaga unga Na mwenzako akimwaga mboga mwaga mafuta Mwanadamu kama hujui ndoa ni mkono karibu na goli Na firimbi imelia golini hamna mtu Lakini goli upana futi moja viatu vimechanika na mpira ni tofari Uwanja kijiji ndani ya nyumba Washangiliaji na wazomeaji wengi sana Maswali mengi kama hayo manung'uniko mengi kama hayo Matatizo mengi kama hayo sasa Yanaonekana ingawa zamani hayakuwako Lakini haya yote yataisha Binadamu wenzangu tambueni dunia hii imegeuka. Kushoto kumekuwa kulia na kulia kumekuwa kushoto Dunia imegeuka ku...