WAHENGA WETU
Waandishi mashuhuri, pamoja na wanachuo
Hodari kwa kufikiri, kutunga yenye mafao
Ilifika safari, kwenda kusiko rejea
Hawakuwa na saburi, wote kwenda zao
Hodari kwa kufikiri, kutunga yenye mafao
Ilifika safari, kwenda kusiko rejea
Hawakuwa na saburi, wote kwenda zao
Walikuwa wapendezi wakifadhili wenzao
Wakapendwa kwa mapenzi, ajabu mfano wao
Kurejea hawawezi, japo tulie vilio
Kwa kilio cha machozi,hawarudi watu hao
Wakapendwa kwa mapenzi, ajabu mfano wao
Kurejea hawawezi, japo tulie vilio
Kwa kilio cha machozi,hawarudi watu hao
Walitenda ya hekima, katika uhai wao
Wakawa wenye kuvuma, kwa sifa zao na vyuo
Kwa hali na taadhima, sifa zikaenda upeo
Wote hayo wamezama, zimebaki sifa zao
Wakawa wenye kuvuma, kwa sifa zao na vyuo
Kwa hali na taadhima, sifa zikaenda upeo
Wote hayo wamezama, zimebaki sifa zao
Comments
Post a Comment