MAISHA MAZURI NI YA MJINI AU VIJIJINI? Uledi nilitembea, mjini na vijijini Ndipo nilipogundua, maisha mema mjini Nakupa zangu hisia, na mawazo akilini vijini ni sulubu, kazi bila maakuli Duka halipo karibu, kilimo na jua kali Maishaye ni adhabu, wakazi hawana hali Pole kwa safari yako, mijini na vijijini Nami nilikuwa huko, nimechunguza makini vijijini mahangaiko, vukumbo na urubini Kule ardhi ni tele, tunajenga kwa nafasi Tunajijengea shule, wakazi sisi kwa sisi Mambo yasonga mbele, kwa mapigo si matusi Mjini njia za lami, viijijini vumbivumbi Mabasi ni kwa makumi, vijijini hawatambwi Mjiji mimi sihami, hapa nimejenga kambi Rafiki yangu miminaona, manufaa kotekote Kote kwasaidiana, vijiji vina matete Si vizuri kuvutana, ili nikuzidi kete Miji na vijiji ndugu, mapacha kwa kuzaliwa Ndugu tusifanye shari, sote tutembeleane Miji na vijiji shwari, bidhaa tuuziane Wewe na mimi kufu, kwa mawazo mwanana Haifai kukashifu, kashifa si mwanana