Skip to main content

DHANA YA MOFU MOFIMU, ALOMOFU NA MAKUNDI YA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

                                       DHANA YA MOFU, MOFIMU NA ALOMOFU
Dhana ya mofu
Mgullu, (1999) anasema kuwa dhana za mofu, alomofimu na mofimu ndizo ambazo hutumiwa sana kwa uchambuzi wa kiisimu hususani katika kiwango cha mofolojia. Istilah hizi zote zimetoholewa kutoka istilahi za kingereza, yaani
a.      Mofu kutoka morph.
b.      Alomofu kutoka allomorph.
c.       Mofimu kutoka morpheme
Inafaa dhana hizi tatu zielezwe vizuri kwa sababu ni dhana muhimu sana katika isimu. Lakini kwa bahati mbaya dhana hizi huchanganywa changanywa sana wakati wa kuzitumia kiasi ambacho kimefanya dhana hizi zionekane kuwa niza kutatanisha siyo katika uchambuzi wa lugha ya Kiswahili tu bali pia hata lugha ya kiingereza ambako zimetokea. Tunasisitiza hapa kuwa dhana hizi zinafaa zielezwe kwa makini na kwa uangalifu wa kutosha ili zisipotoshwe kama ambavyo watu wengine wamekua wakizipotosha.
Dhana ya mofu         
Kama tulivyoeleza apo juu kwa mofu ni istilahi ambayo imetoholewa kutoka istilah morph kutoka lugha ya kiingereza Nida (1949) anaeleza kuwa, Mofu ni umbo la neno ambalo huwakilisha mofimu ambalo hudhihirika kifonolojia na kiothografia. Mofimu ambazo ni elementi dhahania huwakilishwa na mofu ambazo hudhihirika ama kifonolojia zikiwa ni sauti za kutamkwa za kutamkwa au kiothografia zikiwa ni alama za kuandikwa. TUKI (1990) wanasemaje kuwa, Mofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilishacho mofimu.
Platt (1985) naye anaeleza ya kuwa mofu ni kipashio kidogo kabisa chenye maana kabisa katika lugha. Mofu haiwezi kugawanywa katika sehemu ndogo zaidi bila kuharibu maana yake. Mofu huwakilisha maana za kileksika na zile za kisarufi.
Fasili hizi tatu zinaeleza mambo ya msingi kabisa kuhusu sifa muhimu zinazopambanua dhana ya mofu sifa hizi ni pamoja na;
Mofu ni sehemu halisi ya neno
Kinachoelezewa hapa ni kuwa  mofu ni maumbo halisi ya maneno ambayo hutamkwa na watu wanapozungumzoa au kuandikwa wakati wanapoyaandika maneno. Kwa hiyo mofu ni umbo halisi ambalo tunaweza kulisikia linapotamkwa na kuliona linapokuwa limeandikwa.
Mofu hudhihirika kifonolojia na kiothografia
Kwa kuwa mofu ni ubo halisi la neno, basi mofu mbalimbali hudhihirika kifonolojia zinapotamkwa na pia kimaandishi zinapoandikwa.

Mofu huiwakilisha maana
Hapa tunasiisitiza kuwa mofu huwakilisha maana fulani. Kwa hiyo katika neno lolote katika mofu zilizopo katika neno. Hii inatufanya tuelewe  kama kila neno huwa na maana fulani basi maaana hiyo lazima itakuwa imewakilishwa na mofu fulani. Hii ina maana kuwa hakuna neno lolote katika lugha yoyote ambalo linaweza kuwa ni neno lenye maana bila kuwa na mofu angalau moja.
AINA ZA MOFU       
Kwa mjibu wa Mngullu (1999) anasema kuwa mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili:
·         Kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu;
·         Kigezo cha mofolojia ya mofu.
Tunapotumia kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu, tunapata aina tatu za mofu, yaani:
a.       Mofu huru
b.      Mofu funge
c.       Mofu tata
Kwa upande mwingine tunapotumia kigezo cha mofolojia au maumbo ya mofu zenyewe tunapata aina mbili za mofu, yaani:
a.       Mofu changamano
b.      Mofu kapa
Kwa mantiki hii tunazo aina tano za mofu ambazo ni:
a.       Mofu huru
b.      Mofu funge
c.       Mofu tata
d.      Mofu-changamano
Mofu Huru
Weber (1985) anasema kuwa mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza kukaa peke yao kama maneno kamili.
Mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yenye maana inayoweza kueleweka bila kusaidiwa na mofu nyingine. Aghalabu, mifano mingi ya mofu huru hupatikana kutoka kwenye vipashio vya lugha, kama ifuatavyo:
a.       Nomino:  {baba}, {kuku}, {sungura}, {ndege}, {dada}, {paka}, nk.
b.      Vivumishi: {safi}, {baya}, {dhaifu}, {zuri}, {imara}, {hodari}, nk.
c.       Viwakilishi:{mimi}, {sisi}, {wewe}, {ninyi}, {yeye), {wao}, nk.
d.      Vielezi:  {upesi}, {haraka}, {sana}, {leo},  {jana}, {juzi}, nk.
e.       Vitenzi: {tafiti}, {samehe}, {arifu}, {sali},  {jibu}, {badili}, nk.
f.       Vihusishi: {ya}, {juu}, {mbele}, {kwa}, nk.
g.      Viunganishi:{na},{halafu}, {bado}, {ila}, {aidha},{pia}, nk.
Kwa mujibu wa mifano hii inadhihirika kwamba Kiswahili kinazo mofu huru nyingi ambazo zimo katika aina zote za vipashio vya lugha. Hivyo, mofu huru ni mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno kamili yanayoeleweka bila kusaidiwa na viambishi.
Mofu funge au Mofu tegemezi
Richards et al. (1985) wanaeleza ya kuwa mofu funge ni kipashio cha kiisimu ambacho huwa hakikai peke yake bali ni lazima kiandamane na mofu nyingine.
Hartman (1972) naye ana mawazo yanayofanana sana nay ale ya Richards et.al (1985). Hartman anasema kuwa mofu funge ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa peke yake kama neno kamili lililo na maana yake bainifu, bali (daima) hutumiwa kama kiambishi tu kinachoambatana na mzizi au viambishi vingine ili kukamilisha neno.
Mofu funge au Mofu tegemezi ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa peke yake kama neno lililo na maana yake kamili; aghalabu mofu funge hutumiwa kama kiambishi tu kinachoambatanishwa na mzizi au viambishi vingine ili kulikamilisha neno husika. Mofu funge ina sifa zake ambazo ni pamoja na:
(a)        Mofu funge haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili.
(b)        Mofu funge ni lazima iambatanishwe na angalau mafu nyingine moja ndipo tupate neno kamili.
         Kutokana na sifa hii ndiyo mdiyo maana wanaisimu wengine huziita mofu hizi kuwa ni mofu tegemezi ambayo ina maana sawa na mofu funge
Mfano:
                     Idadi ya Umoja          Idadi ya Uwingi
a.       m-toto (m)                 wa-toto (wa)
b.      ki-su (ki)                    vi-su (vi)
c.       m-ti (m)                      mi-ti (mi)
         Ukumbwa wa Nomino           Udogo wa Nomino
a.       ji-tu (ji)                                  ki-ji-tu (ki)
b.      ji-su (ji)                                  ki-ji-su (ki)
Maana za mofu funge hutegemea sana muktadha wa mofu funge husika. Mofu funge ikiondolewa kwenye muktadha wake hukosa maana na ni vigumu kujua maana yake bila kuiweka katika muktadha wa neno. Mofu funge inaponing’inizwa peke yake haituwezeshi hata kidogo kujua maana yake. Umbo moja linaweza kuwa na maana nyingi kwa mujibu wa miktadha ambamo imeambatanishwa katika mzizi wa neno.
Aghalabu, mofu funge ni sawa na viambishi vya mizizi mbalimbali katika neno. Hii ina maana kwamba viambishi vilivyo vingi katika lugha huwa ni mofu funge. Tunasema viambishi vingi kwa sababu si viambishi vyote ambavyo huundwa kwa mofu funge. Vipo viambishi vingine ambavyo huundwa kwa mofu huru. Baadhi ya mizizi ya maneno pia huwa ni ya mofu funge kwa sababu mizizi hiyo huwa haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili. Mifano mizuri ya mizizi ya maneno ya Kiswahili ambayo huundwa kwa mofu funge ni ile ya vitenzi vya silabi moja moja, kama ifuatavyo kwa mfano:
       Mofu funge             Neno                  Mofu funge        Neno
a.       {-l-)                  kula                            {-p-}               mpe
b.      {-j-}                kuja                            {-ny-}            kunya
c.       {-f-}                kufa                            {-nyw-}          kunywa
d.      {a}   {me}   {m}   {nyw}   {esh}   {a}  amemnywesha
Mizizi ya vitenzi hivi ni mizizi ya mofu-funge kwa sababu haiwezi kutumiwa peke yake kama neno na, pia maana zao huwa hazijitokezi mpaka mizizi iwekewe viambishi.
(iii)   Mofu Tata
Mofu tata ni mofu ambazo huwa na maana zaidi ya moja au kuanzia mbili na kuendelea.
Mfano:
Saidi alimpigia Mbaraka mpira.
Sentensi hii ni tata kwa sababu ina maana zaidi ya moja.  Utata wa sentensi hii haupo kwenye muundo wake wa kisarufi, bali upo katika kitenzi alimpigia.  Kitenzi hiki kina mofu sita, yaani:
{a-} + {-li-}  + {-m-} + {-pig-} +  {-i-}   + {-a}
1            2             3             4               5             6
Kati ya mofu hizi zote sita, mofu ya tano {-i-} ndiyo yenye utata. Mofu {i} ni mofu ya kutendea kwa sababu tukisema: ‘Saidi alimpigia Mbaraka mpira’, maana zinazoweza kueleweka na wasikilizaji ni nne:
a.       Saidi aliupiga mpira kwa niaba ya Mbaraka; yaani Mbaraka ndiye aliyetakiwa aupige mpira ule, lakini kwa sababu ambazo hazikuelezwa, badala ya Mbaraka kuupiga mpira ule, Saidi akaupiga.
b.      Saidi aliupiga mpira kuelekea kwa Mbaraka; yaani Saidi na Mbaraka walikuwa wakicheza mpira. Ikapatikana fursa, Saidi akaupiga mpira ule kuelekea kwa Mbaraka. Kwa hiyo, hapa tunazungumzia mwelekeo wa mpira.
c.       Saidi alimpiga Mbaraka kwa kuutumia mpira; yaani, Saidi anautumia mpira kama ala (silaha) ya kumpigia Mbaraka.
d.      Saidi alimpiga Mbaraka kwa sababu ya mpira; yaani hapa, mpira ndio sababu kubwa ya Saidi ya kumpiga Mbaraka. Tuseme labda Saidi alikuwa na mpira wake, halafu Mbaraka akauchukuwa kuuchezea na kwa bahati mbaya akaupoteza. Saidi anapogundua kwamba Mbaraka ameupoteza mpira wake, basi ndipo akampiga.
Kwa maelezo hayo, ni wazi kwamba sentensi yetu ina utata kwa kuwa inatupatia maana tofauti tofauti zipatazo n’ne ambazo zimesababishwa na mofu {-i-} ya kutendea.


(iv)      Mofu Changamani
Mofu changamani ni mofu ambazo huundwa kwa kuweka pamoja angalau mofu-sahili mbili au mofu funge na mofu sahili yakafanyiza neno lenye kuleta maana kamili, kwa mfano:
                                Mofu sahili + Mofu sahili
a.                   {askari} + {kanzu} = askari kanzu.                        
b.                  {gari} +  {moshi} =  gari moshi.
c.                   {paka} + {shume} = paka shume.
d.                  {m’mbwa} + {mwitu} = m’mbwa mwitu.      
e.                   {fundi}   {chuma} = fundi chuma
                                   Mofu funge   +   Mofu huru            
a.         {mw} + {-ana}+       {nchi}             mwananchi.         
b.       {ki} + {-on-} + {a}  +          {mbali}=  kiona mbali.
c.        {mw} + {-ana}+       {hewa }=  mwanahewa. n.k     
(v)       Mofu Kapa
Mofu kapa ni mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno, lakini athari zinazotokana na hiyo mofu kapa husika hueleweka. Ingawa mofu hizi huwa hatuzioni wala kuzitamka au kuziandika, lakini maana zake tunazipata. Tukichunguza ruwaza ya viambishi awali vya umoja na wingi katika lugha ya Kiswahili, tunaweza kuzigawa nomino za Kiswahili katika makundi makuu man’ne, yaani:
   Nomino zilizo na viambishi bayana vya idadi ya umoja na uwingi:                
Mfano:
Umoja            Wingi
a.       m - tu              wa - tu
b.      m - toto           wa - toto
c.       m - ti               mi – ti
 Nomino zilizo na kiambishi awali cha umoja tu, cha wingi hakipo, kwa hivyo, ni kapa  (φ)
Mfano:          
Umoja                        Wingi
a.       u - kuta                      φ - kuta
b.      u - funguo                  φ - funguo
c.       u – kucha                   φ – kucha.
  Nomino zilizo na kiambishi cha wingi tu, cha umoja hakipo; kwa hivyo, ni kapa (φ)
Mfano:
Uoja                        Wingi
a.       φ – kasha                 ma – kasha.
b.      φ – debe                    ma – debe.
c.       Φ – jembe                 ma – jembe.
 Nomino zisizo na kiambishi awali cha umoja wala cha wingi
Mfano:
Umoja                        Wingi
a.       θ - mama                    θ - mama.
b.      θ - ng’ombe                θ - ng’ombe.
c.       θ - baba                      θ - baba.       
d.      θ - kaka                      θ - kaka.
e.       θ - dada                      θ - dada.
f.       θ - mbuzi                    θ - mbuzi.
g.      θ - ngamia                  θ  - ngamia.
h.      θ - kondoo                  θ  - kondoo.
i.        θ - tembo                    θ - tembo.
j.        θ - sungura                 θ  - sungura.
k.      θ - nguruwe               θ  - nguruwe
 (e)     Sherehe kuhusu Mofu kapa
Katika kuonyesha mofu kapa tutatoa sherehe kuhusu makundi haya Katika makundi hayo hapo juu nomino zina kiambishi awali cha umoja tu, wakati cha wingi hakipo. Kinachotokea hapa ni kwamba ukisema ukucha watu wanaelewa kuwa ni ukucha mmoja tu. Lakini ukisema kucha,  watu wataelewa kuwa ni kucha nyingi. Na hali hii ndivyo ilivyo kwa maneno ufunguo  ǂ  funguo;  ukuta ǂ kuta, nk. inajulikana kuwa ni ufunguo mmoja tu na akisema funguo, ni kwa maana ya wingi; lakini umbo lenyewe linaloileta hiyo maana ya wingi halionekani bayana katika neno. Ili kuyaeleza haya maumbo ambayo hayapo lakini maana zinazowakilishwana maumbo hayo zipo, Wanaisimu wamekubaliana kuyaita maumbo  haya kapa, yaani mofu ambazo hazipo. Mofu hizi ni dhahania tu katika akili zetu kwa kufahamu tu kwamba maana fulani haiwezi kuja tu yenyewe lazima iletwe na mofu fulani. Kwa hivyo, hata kama mofu hiyo haionekani, lakini ipo; ni mofu-kapa.
Kwa mfano, katika matamshi ya maneno: kasha, debe, jembe, umoja na uwingi wake hudhihirishwa kama ifuatavyo:
        Umoja                        Uwingi
a.       kasha                          makasha
b.      debe                            madebe
c.       jembe                         majembe
Katika nomino hizi mofu ya uwingi ni mofu  {ma} lakina mofu ya    umoja ni mofu kapa, yaani haipo na huoneshwa kwa alama {Φ}.
Kwa mantiki hiyo, mofu za maneno haya ni kama ifuatavyo:
Umoja                        Uwingi
a.       {θ } + kasha              {ma} + {kasha}
b.      { θ } + debe                {ma} + {debe}
c.       {θ}+jembe                  {ma}+{jembe}

Dhana ya mofimu
Ingawa katika kazi hii kuieleza dhana ya mofu lakini historia inaonyesha kuwa histilahi ya mofimu ndiyo iliyoanza kutumiwa kabla istilahi ya mofu. kwa mujibu  wa  crystal  (1971)  wakati  wa  sarufi  mapokeo  ( traditional grammar)  uchambuzi  wa kiisimu. katika kipindi hiki  sentensi iligawanywa  ( segmented)  katika vipashio  vidogo vidogo kama vile vishazi , virai na hatimaye neno. lakini baadaye katika karne za 18 na 19 ilibainika  kuwa palikuwa na  haja ya kwenda  chini zaidi yaneno. wakati huu ndipo istilahi ya  mofimu  ilipoanza  kutumika .mofu  ilianza kutumika   baadaye  zaidi katika  karne ya 20  hasa baada ya  kuasisiwa  kwa sarufi zalishi. Dhana ya mofimu ina sura kuu mbili zinazo tofautiana sana. sura hizo zinalingana na vipindi vikuu viwili ambamo dhana hii ilitumika,yaani:
a.       Dhana ya mofimu ya kusisiwa kwa sarufi zalishi.
b.      Dhana ya mofimu baada ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi.
c.       Dhana ya mofimu kabla ya sarufi zalishi       
Wanaisimu walipoona umuhimu wa kuwa na kipashio kidogo zaidi ya neno katika uchambuzi mara walibuni na kuanza kuitumia dhana ya mofimu. Badala ya uchambuzi kuishia kwenye neno tu, uchambuzi ukawa unaendelea hadi kwenye kiwango cha mofimu. kwa mfano sentensi kama :
“Tumaini anakata miti” Ingechambuliwa kama ifuatavyo :
Uchambuzi kabla ya sarufi zalishi
            S          sentensi


                                                     KN                                                    KT    vikundi / virai


                                                         N                                      T                        N  maneno


                                                     Tumaini                  anakata                    miti




                   Uchambuzi baada ya kuasisiwa sarufi zalishi
                                                     S                               sentensi


                                                      KN                                                   KT    vikundi / virai


                                                         N                                      T                        N  maneno


                                                        Tumaini               anakata              miti
Katika uchambuzi wa awali sentensi imegawanywa katika sehemu kuu mbili yaani:
1. kiima (Tumaini) 2.kiarifu (alikata miti)  kiima kina nomino moja  (Tumaini) na kiarifu kina kitenzi na nomino (miti) sentensi ni mfululizo wa maneno matatu. katika uchambuzi wa baadaye sentensi imegawanywa katika: kiima na kiarifu, kiima kina nomino moja (Tumaini), kiarifu kina kitenzi (alikata) na nomino (miti), Nomino Tumaini ina mofimu moja tu (Tumaini), kitenzi alikata kina mofimu nne ({a}+{ li } +{ kat} +{a}, Nomino miti ina mofimu mbili (mi) + (ti) Sentensi ni mfululizo wa mofimu saba (7)
Dhana ya mofimu katika kipindi cha kabla ya sarufi zalishi ni sawa na dhana ya mofu tulivyoieleza hapo juu katika sehemu ya mofu. Yale yote tuliyoyasema kuieleza mofu ndiyo ambayo tungeweza kuyatumia hapa kuieleza dhana ya mofimu kabla ya sarufi zalishi. Miongoni mwa wale wanaoitazama dhana ya mofimu kwa jicho hili la awali ni watu kama Crysstal (1971), Mohamed (1986), Richards et al, (1985), Kayuza (1988) na Maarealle (1971), Crystal (1971), kwa mfano, anasema kuwa:
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa katika lugha chenye maana zaidi ya hayo, maana hiyo hutofautiana na zile za mofimu zingine katika lugha hiyo. Mambo mawili yanabainika hapa. Kwanza ni kuwa ukiongeza au kupunguza mofimu kutoka tamko fulani, bila shaka maana ya tamko itabadilika.
Crystal (1971) anaendelea kusema: Kwa hiyo mofimu inazo sifa kadhaa zinazoibainisha, na tatu kati ya sifa hizo ni muhimu. Kwanza, mofimu ni kipashio chenye umbo halisi. Mofimu ina umbo lake la kifonetiki. Pili, mofimu huwa na maana. tatu, kila mofimu huwa na nafasi yake ya kisintaksia katika (kushirikiana na vipashio vingine) Kuunda vipashio vikubwa zaidi. 
Maelezo ya mofimu anayoyatoa Crystal yanaafikiana nay ale tuliyoyatooa kuhusu mofu katika sehemu inayotangulia. Utadhani mofu ni sawa na mofimu. Marealle (1978) naye hatofautiani na Crystal (1971) katika kuifafanua mofimu. Yeye anasema: Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha kisarufi kilicho na maana. Marealle anatoa mifano ya mofimu katika maneno yafuatayo ya Kiswahili
A-na-tembea (mofimu4) 2. A-na-kimbi-a (mofimu 4)
Marealle sawa na Cystal (1971) anasema kuwa mofimu ni maumbo madogo kabisa ya maneno yenye maana. Kumbuka kuwa maelezo haya ni sawa na maelezo yetu tuliyoyatoa kuhusu mofu. Mohammed (1986) naye ana mawazo sawa na Crystal na marealle. yeye anasema kuwa: Hivyo basi, mofimu ni kijineno au sehemu ndogo ya tamko iletayo maana kamili ya kisarufi.
Mohammed (1986) anatoa mfano wa neno anapika. Analigawa neno hili katika vile anavyoviita vijineno (mofimu) vifuatavyo: a-na-pik-a. Tunaona hapa kuwa dhana ni ile ile ya sehemu ndogo kabisa ya neno yenye maana. Hata hivyo, maelezo ya Mohamed yanaweza kuleta neno yenye maana. Hata hivyo, maelezo ya Mohammed yanaweza kuleta utata. Kwa mfano kuna uhalali gani wa kuziita mofimu kuwa ni vijineno? je (a) ni kijineno? maana ya neno na kijineno ni nini hapa? pia kuna utata anaposema kuwa mofimu huleta maana kamili ya kisarufi. Maana zinazoletwa na mofimu ni za aina mbili, ama za kileksika au za kisarufi. Hatuelewi ni kwa nini mohammed ameibana fasili yake katika maana za kisarufi tu. Hata hivyo, mfano wake unatusaidia kujua anachotaka kueleza. Kaayuza (1988) naye yumo katika kundi lili hili. Yeye anasema kuwa:
Mofimu ndiyo ngazi ya mwisho ya maumbo. Mofimu ni tamko dogo lenye maana ya kisarufi. kwa mfano:
Sentensi: Juma a- na- lim-a     shamba
Mofimu:           1    2   3   4     5     6
Ingawa maelezo yake yana upungufu, lakini mfano wake umetusaidia kuelewa kile kilicho akilini mwake. TUKI (1990) nao wametumbukia katika mtego huu huu. Wao wanasema:
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa amilifu katika maumbo ya maneno.
Kama tulivyokwisha kusema, maelezo haya yote ni sawa kabisa na yale tuliyoyatoa kuhusu mofu. Hawa wanaiona mofimu kuwa ina maana sawa na mofu. tunachoweza kusema ni kuwa maelezo haya yanaiona mofimu kama kipashio alisi cha neno kilicho na umbo lake la kifonetiki (wakati maelelezo yanaiona mofimu kuwa ina maana. Ni maelezo yaiyotumiwa kabla ya kuundwa kwa dhana ya mofu. Baada ya kuundwa kwa dhana ya mofu maelelzo haya ya mofimu kama kipashio chenye maana yalihamishiwa kwenye mofu a mofimu ikapewa maana mpya.
Kilicho bayana ni kuwa kama wakati wa sasa ambapo tunazo istilahizote mbili, yaani mofu na mofimu, tutaieleza mofimu kama kipashiop kidogo kabisa cha neno chenye maana. je mofu tutaieleza kuwa ni nini? hufanya dhana za mofu na mofimu zionekane kama zinafanana, au zinatatanisha.



Dhana ya mofimu baada ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi
Baada ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi katika karne ya 220, dhana muhimu mbili ziliingizwa katika uchambuzi wa mofolojia ya lugha. Dhana hizo ni mofu na alomofu. Dhana ya mofu imeelezwa hapo juu na hivyo ndivyo inavyopaswa ieleweke hadi leo. dhana ya alomofu itaelezwa baadaye. Maana iliyokuwa imepewa mofimu, kama kipashio kidogo kabisa cha lugha kinachobeba au kusitiri maana. (rejea sehemu ya mofu). Sasa mofimu ikapewa maana mpya. Fasili mojawapo inayotoa hii maana mpya ya mofimu ni ile ya Hartman (1972) ambaye  anasema kuwa: Mofimu ni kipashio dhahania cha umbo fulani ambacho kinaweza kuwakilishwa na mofu tofauti tofauti katika mazingira anuwai. mofimu ya wingi katika lugha ya kiingereza, kwa  mfano, huwakilishwa na mofu  /s/, /z/, /iz/ na kadhalika.
Lightner (1975) naye anaeleza ya kuwa: Kwa kweli mofu imo katika upande wa utendaji lakini mofimu ni dhana ya kidhahania iliyomko akilini mwa watu na ambayo ni sehemu ya umilisi wa lugha wa kila mtu. Mofimu ni tafsri ambayo mtu huifanya akilini mwake kuhusu maana ambayo husetiriwa kwenye mofu.
Fasili hizi mbili zimepiga hatua kubwa kwa sababu zimefaulu kutofautisha dhana ya mofu na mofimu. Fasili hizi zina mambo muhimu tunayoyajadili hapa chini.
Mofimu ni kitu dhahania
Hapa tunapewa ile tofauti ya msingi kuwa wakati ambapo mofu ni sehemu halisi ambazo huwa tunazitamka au kuziandika tunapoandika maneno lakini maana ambazo huwakilishwa na mofu hizo ambazo ndizo tunazoziita mofiu bhuwa ni dhahania kwa sababuy maana hizo huwa hazitamkwa wala kuandikwa. Maana hizo huwa akilini mwa watu. Hapa kuna tofauti kati ya maana (mofimu) na namna ya kuziwakilisha maana mofimu (maana) ya wingi  katika ugha ya kiingereza huwakilishwa na maumbo mbalimbali kama /s/, /z/, /iz/, na kadhalika. Tungeweza kuendeleza hapa kuwa hata katika lugha ya Kiswahili mofimu ya wingi huwakilishwa na mofu kadhaa kutegemea aina ya nomino inayowekewa wingi. Kwa mfano, kuna:
a.       Mofu {wa} katika nomino kama {wa} + toto, {wa} + tu, {wa} + alimu, {wa}+ ungwana,
b.      Mofu {mi} katika nomino kama {mi} + kono, {mi}+ti+chungwa, {mi}+tume, {mi}+jusi,
c.       Mofu {ma} katika nomino kama {ma} + cho, {ma} +we, {ma} +no (meno), {ma}+iko (meko), {ma} +jemadari, {ma} +jambazi, n.k.
d.      Mofu  {vi} katika nomino kama {vi}+ atu, {vi} +ti, {vi} +ti  {vi} +tu, {vi} +azi, {vi} +tanda, {vi} +ongozi, {vi}+ jana, {vi}+pofu,
e.       Mofu {Ɵ}/ {Kapa} katika nomino kama Ɵkuta, Ɵkucha, Ɵfunguo, Ɵpawa, Ɵ pande, Ɵkuni, n.k.
Kwa hiyo hii mifano inaonyesha kuwa, maana (mofimu) ile ile ya wingi inaweza kuwakilishwa na maumbo {wa}, {mi}, {ma}, {v}, na {Ɵ}.
Maumbo haya yote yanapotumika katika mazingira yanayofaa huwa yamesetiri ile maana ya wingi. Kwa Mantiki hiyo mofimu si sehemu iliyopo kwenye neno. Mofimu haziwezi kuhesabika kwani si vitu halisi ni vitu dhahania. Ni sawa na mtu anapozungumzia maneno na maana zake. Neno huonekana likatamkwa na kuandikwa. Neno ni sehemu ya utendaji (performance) na neno lipo upande mmoja na mofu. Lakini maana za maneno ni dhahania, zipo akilini mwa watu. Maana za maneno huwa hazitamkwi wala kuandikwa na awatu. Lakini maana hizo huwa akilini mwa watu wanaozungumza na kusikiliza nah ii ndiyo maana watu hawa huelewana. Maana za maneno zipo upande mmoja na maana za mofu ambazo tunaziita mofimu. waandishi kama marealle (1978) na Kayuza (1988) wanafanya makosa makubwa wanapodhani kuwa mofimu ni maumbo ya maneno yenye maana ambayo tunaweza kuyahesabu. marealle (1978), kwa mfano, anasema kuwa neno anakimbia lina mofimu nne na anazionyesha:
a+ {na} + {kimbi} + {a}
1         2          3           4
Haya si maelezo sahihi. Kayuza (1988) naye anasema kuwa sentensi “Juma analima shamba” ina mofimu sita na anazionyesha.
(Juma) + (a) + (na) + (lim) + (a)  + (shamba)
1              2       3        4         5           6
Mtazamo huu pia si sahihi. Ama kwa hakika, hizi zote wanazoziita mofimu ni mofu na mofimu ni maana zilizomo kwenye mofu hizo. maana (mofimu) zilizopo katika sentensi “Juma analima shamba” ni hizi zifuatazo.
MOFU                                                MOFIMU
1.      {Juma}                       (1) Mtu, (2) Idadi: mmoja, (3) Jinsia: mwanaume
2.       {a}                            (1) Kipatanishi, (2) Nafsi ya tatu,  (3) Idadi: Mmoja
3.        {na}                       (1) Njeo: sasa,  (2) Hali: Kuendelea
4.       {lim}                        (1) Mzizi wa kitenzi
5.       {a}                              (1) Kiambishi tamati,  (2) Kauli ya kutenda,  (3) Yakinishi
6.      .{Ɵ} (kapa)                   (1) Idadi ya umoja
7.       {Shamba}                     (1) Mzizi wa nomino
                                                   (2) Ardhi kubwa kuliko inayolimwa kupanda maua.
Kwa ufupi tunaona mofimu (maana) mbalimbali tunazozipata kutokana na mofu saba kuwa ni kumi na tano (15). Huu ni uthibitisho mwingine kuwa yale ambayo humjia mtu akilini anaposikia tamko fulani, yaani mofimu za mofu ni, mengi. Ingawa mofu zipo saba tu lakini mofimu ni kumi na tano. Mofimu hapa si maumbo ya maneno bali ni maana tunazozichuja akilini mwetu. Tunapenda tusisitize hapa kuwa tangu dhana ya mofu ilipoanzishwa baada ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi dhana ya mofu imepewa fasili iliyokuwa ya mofimu na dhana ya mofimu ikapewa fasili mpya. kwa sasa mofu ndiyo inayopewa maana ya:
Kipashio kidoo kabisa cha kimofolojia kinachosetiri maana. Kipashio hiki ni halisi na hudhihirika kifonetiki na kiothografia.
Nayo mofimu kwa sasa hupewa ile maana ya dhana ya kidhahania ambayo ni maana ambayo/zo huwakilishwa au kusetiriwa katika mofu. Tumetumia muda mrefu kuieleza hii dhana ya mofimu kwa sababu ndiyo kwenye matatizo zaidi kwa sababu mara nyingi huwa inachanganywa na mofu kiasi kuwa mtu atashawishika kudhani kuwa mofu (umbo) ni sawa na mofimu (maana). Labda wakati mwingine makosa haya yanatokana na watu wengine kutokujua kuwa maana ya mofimu imebadilika sana.

Hivyo tunaweza kusema kuwa kabla ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi dhana ya mofimu ilichua maana ya mofu kama ilivyojadiliwa katika sehemu iliyotangulia hapo juu. Lakini baada ya kuasisiwa srufi zalishi mofimu ina maana inayowakilishwa na mofu hivi kwamba mofimu ni dhana dhahania ambayo ni sehemu ya umilisi wa mtumiaji wa lugha husika kutokana na fasili hii mofimu ni lie maana iliyowakilishwa na mofu. Kwa misingi ya mantiki mofu ni sehemu halisi, hutamkika, huandikika na kuonekana ilhali maana mofimu ni dhahania na huwa imo akilini mwa mtumiaji wa lugha husika.
Lakini katika fasili ya Habwe na Karanja (2004) wanaposema kuwa uhusiano kati ya mofu na mofimu  ni ule wa umbo na yaliyomo au kiashiria na kiashiriwa.
Kwa mfano,
1.      {a}+{na}+{pik}+{a}
Mofu {a-} huwa na mofimu zifuatazo
a.       Mtenda
b.      Nafsi ya tatu umoja
c.       Kiambishi kipatanishi cha kisarufi cha ngeli ya kwanza
Kutokana na mfano huu mofu inaweza ikawa moja lakini  zikawa zaidi ya moja.


DHANA YA ALOMOFU
Dhana ya alomofu.
Baada ya kueleza dhana za mofu na mofimu tunaweza sasa kueoleza dhana ya alomofu. Richards et al (1985) wanaeleza vizuri kuwa:
Alomofu ni umbo mojawapo kati ya maumbo kadhaa tofauti yanayoiwakilisha mofimu moja.
 Hartman (1970) naye anasema kuwa: Alomofu ni umbo badala la mofimu fulani ambalo halibadili maana. Katika lugha ya kiingreza, kwa mfano, kiambishi tamati /s/ cha wingi kina maumbo badala yafuatayo:
a.       /s/ kama  katika maneno cats, books, n.k.
b.      /z/ Kama katika maneno dogs, bags, n.k.
c.       /iz/ kama katika maneno classes, boxes, n.k
d.      / Ɵ/ kama katika neno sheep.
Bauer (1983) naye anasema kuwa: Alomofu ni mofu mojawapo katika seti ya mofu zinazoiwakilisha mofimu fulani ambayo ina mazingira yake ya kifonetiki, kileksika au kisintaksia (kisarufi).

Alomofu ni umbo badala la mofimu fulani ambalo halibadili maana. Katika lugha ya kiingreza, kwa mfano, kiambishi tamati /s/ cha wingi kina maumbo mbadala. Alomofu hufafanuliwa kama maumbo zaidi ya moja (mbalimbali) ya mofimu moja.
Neno alomofu linatokana na maneno mawili ambayo ni “alo” lenye maana ya zaidi ya moja au mbalimbali na “mofu” lenye maana ya umbo.
Mfano
a.       M (u) +tu: wa+tu
b.      M (u) +ke: wa+ke
c.       Mw+alimu: w+alimu
d.      Mw+anajeshi: w+anajeshi
Katika mifano hiyo //mu// ya umoja ina maumbo mawili ambayo ni //m// na  //mw// halikadhalika //wa// ya wingi nayo ina maumbo mawili ambayo ni  //wa// na  //w//  hivyo maumbo haya yanaweza kuelezwa kwa kanuni ifuatayo:
//mu//------->[m]/-k
------->[mw]/-I
//wa//-------->[wa]/-k
------->[w]/-I
Fasili tatu tulizozitoa hapo juu zinaeleza sifa muhimu zinazoifafanua alomofu. Sifa hizo niL
Alomofu ni umbo
Kama ilivyo kwa mofu, alomofu ni umbo halisi ambalo ni sehemu neno fulani na ambalo hutamkwa na kuandikwa. kwa hiyo alomofu ni mofu na sifa tuizozitoa kuhusu mofu ndizo zinazofaa pia kuelezea alomofu.
Alomofu ni mofu mojawapo miongoni mwa mofu za mofimu moja
Tofauti iliyopo kati ya mofu na alomofu ni ndogo sana. Tofauti hiyo ni kuwa mofu huwa ni mofu wakati ambapo umbo moja tu hutumika kuiwakilisha mofimu fulani. Aghalabu mofu ambazo ni mizizi ya maneno, au tuseme mofu za kileksika huwa na umbo (mofu) moja tu ambalo huwakilisha kitu fulani na mofu hizo huendelea kuitwa mofu za momifu fulani kwani zina sura moja tu. popote zinapotokea hutokea na sura hiyo hiyo na hazibadiliki. tutoe mfano wa mofu (imb). (imb) hubakia tu mahali popote inapotokea kama:
a.        Imb+ a                                        (imba)
b.      si+imb+i                                      (siimbi)
c.       u+si+imb+e                                  (usiimbe)
d.      tu+ta+ imb+a                               (tutaimba), n.k.      
Wakati mofimu fulani inapokuwa na umbo moja tu linaloiwakilisha mofimu hiyo, umbo hilo moja huitwa mofu. Lakini, wakati mwingine mofimu moja huweza kuwakilishwa na mofu (maumbo) kadhaa. katika hali kama hii mofimu inakuwa ni moja lakini maumbo (mofimu yanayoiwakilisha mofimu hiyo yanakuwa mengi basi kila mofu miongoni mwa mofu hizo kadhaa za mofimu moja itaitwa alomofu badala ya kuitwa mofu. Hii inatuonysha au kutumumbusha kuwa hili ni umbo mojawapo mofu huwa hazina mazingira (contex free), yaani kila mahali zinapotokea huitokea na umbo hilo hilo, alomofu kwa upande wake zinatokea katika mazingira maalumu. kwa maneno mengine alomofu zimegawana mahali pa kutokea, yaani mgawanyo wa kiutoano (complementary distribution) hasa kwenye mipaka ya mofu hizo kiasi kwamba umbo la awali la mofu ya kuathiriana tuliite umbo la ndani,  huwa ni tofauti na lile umbo linlotokea baada ya kuathiriana tuliite umbo la nje. Tunaona, kwa mfano katika lugha ya Kiswahili wakati mwingine maumbo ya ndani nay a nje ya mofu huwa tofauti,
 Kwa mfano
              Umbo la ndani              Umbo la nje
a.       {lind}  (linda)              {linz} (mlinzi)
b.      {chek} (cheka)             {chesh} (mcheshi)
c.       {Pend} (penda)                {penz} (mpenzi)
d.      {u}+{ema}                   (wema )
e.       {pik} (pika)                  {pish} (mapishi)
f.       {ing} (mu+igo)             {mw} (mwigo)
g.      {ma} ma+ingi)             {me} (mengi)
h.      {vi} (v+ote)                 {vy} (vyote)
Wataalamu wa mofolojia ya kiingereza, kwa mfano, wanaweza kueleza ni katika maneno yapi mofu/s/ ya wingi itatumika na ni wapi mofu/z/ itatumika. Watakueleza, kwa mfano, kuwa mofu/s/ hutumika katika maneno yanaoiishia na obstruenti hafifu (voiceless obstruents) mofu /iz/ hutumika aktika maneno yanayoishia na konsonanti vifyonzo (sabilanti consonants) kama /s, z, dz/. Na mofu /z/ hutumika katika sehemu zingine zote zilizosalia la muhimu tunalosema hapa ni kuwa kiila alomofu ina mazingira yake ya kifonetiki, kileksika na kisintaksia. Alomofu hazitumiwi ovyo ovyo tu.

MAZINGIRA YA UTOKEAJI WA ALOMOFU
Alomofu hutokea katika mazingira maalumu. Mazingira mengine yanatabirika na mengine hayatabiriki. Hata hivyo, alomofu huweza kutokea katika mazingira ya aina tatu ambayo ni:,
·         Mazingira ya kifonolojia
·         Mazingira ya kileksika (kikamusi)
·         Mazingira ya kisarufi





Mazingira ya kifonolojia
Mazingira ya kifonolojia ya utokeaji wa alomofu hujitokeza pale ambapo maumbo fulani hutokea kama alomofu kutokana na athari za kifonolojia.
Mfano  
M [u]/ -k
  Mu                  mw/-I
Mifano hiyo inaonesha jinsi umbo moja linavyoweza kubadilika na kuwa katika muonekano tofauti huku maumbo yote hayo yakiendelea kubeba taarifa ileile. Mabadiliko haya huwa yamesababishwa na athari za kifonolojia za sauti fulani.
 Umbo  “mu” linatokea kama //mu// au //m// linapofuatwa na konsonanti na linakuwa  umbo //mw// linapofuatwa  na irabu.
Vilevile umbo //wa// linalojitokeza kama //wa// linapofuatwa na konsonanti  na linakuwa //w// linapofuatwa na irabu.
Vilevile mazingira ya kifonolojia hujidhihirisha katika utendaji. Utokeaji wa alomofu za kauli huwa katika mazingira yanayotabirika na yasiyotabirika.
Mazingira yanayotabirika ya utendea
Mfano:1
a.       Funga – fung+i+a
b.      Lima – lim+i+a                   {- i-}
c.       Paka – pak+i+a
Mofu ya utendea {-i-} hutokea iwapo mzizi umebeba irabu a, i, u.
//utenda//------->{- i-}/- mzizi [ a, i, u]
Mfano:2
a.       tema  - tem+e+a
b.      soma  - som+e+a                 {-e-}
c.       c) enda  - end+e+a
Mofu ya utendea {-e-} inatokea iwapo mzizi umebeba irabu e au o
//utendea//-------->{- e-}/- mzizi [e, o]
Mfano:3
a.       Chukua - chuku+li+a
b.       Kimbia - kimbi+li+a               {- li-}
c.        Pakua   - pak+u+li+a
Mofu ya utendea {-li-} hutokea iwapo mzizi una irabu a, i, u.
//utendea//-------->{-li-}/- mzizi mf I [a, i, u]

Mfano:4
a.       Zoa   - zo+le+a
b.       Toa   - to+le+a                        {-le-}
c.       Toboa – tobo+le+a
Mofimu ya utendea {-le-} inatokea iwapo mzizi una irabu e au o.
//utendea//-------->{-le-}/- mzizi mf I [e, o]
Mazingira ya utokeaji wa alomofu ya utendeshi.
Mazingira yasiyotabiriki. Mfano
a)      lala-laza
b)      shuka-shusha
c)      lewa-levya
d)     ogopa-ogofya
e)      gawana-gawanya
Alomofu za utendeshi ni z, sh, vy, fy, ny.
Mazingira ya kileksika
Utokeaji wa alomofu katika mazingira ya kileksika huwa tunazingatia ngeli za nomino kupitia mofu za umoja na wingi za nomino husika.
  Mfano
a)      Kijana    vijana
b)      Mtume     mitume
c)      θRaisi    maraisi
d)     θMungu    θMungu
     Katika mifano hiyo;
Alomofu za umoja ni ki, m, θ
Alomofu za wingi ni, vi, mi, ma, θ
//umoja//----> ki /-konsonanti
//wingi//----> vi/-k
//umoja//----->{m}/-k
//wingi// ---->{mi}/-k
//umoja//----> { θ}/-raisi
//wingi//----->{ ma}/-raisi
//umoja//----->{ θ}/-Mungu
//wingi//------>{ θ}/-Mungu.
Mazingira ya kisarufi

Mfano
a)      anapika - hapiki
b)      alipika - hakupika
c)      atapika - hakupika
d)     amepika - hajapika
a.       Alomofu za njeo ni:-na, li, ta, me, i, ku, ja
b.      Alomofu za njeo uyakinishi ni; na, li, ni, ta, me
c.       Alomofu za njeo ukanushi ni; i, ku, ta, ja

VIGHAIRI
Vighairi ni dhanna inayohusu alomofu ambazo utokeaji wake   haufungamani na kanuni wala masharti yoyote.
Mifano
(a)      ki+tabu  -  vi+tabu
(b)      ki+jiko  -  vi+jiki
(c)       ki+nu    -  vi+nu
(d)     ch+umba  -  vy+umba
(e) ch+eti   -  vy+eti
(f) ki+oo    -  vi+oo
(g) ch+oo    - vy+oo
(h) ch+umba  - vy+umba
Mifano hiyo //ki// ya ngeli ya KI-VI umoja ina alomufu //ki-// na //ch-// na mofu //vi-// ya wingi ina alomofu //vi// na //vy//.
ZINGATIA: Maneno choo, vyoo, chumba, vyumba, chetu, vyetu, ni vighairi kwa sababu yanashiriki ngeli ya KI-VI lakini hayakubali mofu //ki-// na //vi-// kukaa mwanzoni. Kimsingi //ch-// na //vy-// zipo kwenye ngeli ya KI-VI lakini mwanzoni zipo zilivyo yaani, ki-vi itatokea tu kwenye kitenzi cha upatanisho wa kisarufi.
Mfano;   choo kimejengwa
Vyoo vimejengwa
KUTENGANISHA MOFU NA ALOMOFU
Lugha ya Kiswahili ni lugha ambishi hivyo ina maneno ambayo huundwa kwa mwandamo wa kisafu wa mofimu. Mofu hizi hupachikwa kabla na baada ya mzizi kwa mfuatano ulio bayana.
Mfano;
     A                               B
(a) Anasoma                    a-na- som-a
(b) Apikiwe                      a-pik-iw-e
(c) Fungana                      fung-an  a
Utenganishaji wa mofu katika maneno hayo unaonekana ni rahisi kwa kuwa miundo ya maneno hayo inafahamika.
Tunapotenganisha mofu za lugha tusiyoijua ni lazima tuwe na miundo yenye ruwaza zinazolingana ili tuweze kufananisha maana na maumbo mapya yanayoandamana na maana mapya.
  Mfano;
(a)    alatambuka  -  atatembea
(b)   Mulatambuka - mtatembea
(c)    Balatambuka - watatembea
(d)   Mukatambuka – mlitembea
(e)     Balayajula -       watatambaa
Ingawa lugha hii yawezekana hatuitambui bado tunaweza kutenga mofu zake kwa urahisi kwa kuwa kuna ruwaza zinazofanana na zile za lugha tunayoifahamu. Kutokana na data ya lugha ya hapo juu (kihaya) kuna mofu zifuatazo.
   Mofu za za:
                    i.            //nafsi//--------- {a} -3-umoja
-------- {mu} -2-wingi
------ {ba} -3-wingi
                  ii.            //njeo//----------- {la} -ijayo
----------- {ka} -iliyopita
                iii.            //mzizi//---------- tambuk -
----------- yajul –
        KANUNI ZA KUTENGANISHA MOFU
 Kanuni ya kwanza; zingatia maumbo yenye maana sawa. Maumbo hayo huweza kufanana au kuhitilafiana kiumbo lakini hutokea katika mazingira yaleyale. Mfano;
a.       Atakupiga    a-ta-ku-pig-a
b.      Atampiga     a-ta-m-pig-a
c.       Alikupiga    a-li-ku-pig-a
d.      Utanipiga    u-ta-ni-pig-a
e.        Utatupiga    u-ta-tu-pig-a
f.       Mlijipiga    m-li-ji-pig-a
Mofu
Mofu nafsi--------- {a}-3-umoja
--------- {u}-2-umoja
---------- {m}-2-wingi
---------- {tu}-1-wingi
Mofu njeo ------------- (ta)-ijayo
------------- {li}-iliyopita
-------------- {na}-iliyopo
Yambwa ---------------- (ku)-wewe
--------- {m}-yeye
---------- {ni}-mimi
----------- {ji}-binafsi
Kanuni ya pili; Hapa kinachozingatiwa ni maumbo yenye maana moja lakini yasiyo na umbo sawa la kimofolojia.
     Mfano;
a.        Mtumwa         watumwa
b.       Mvulana        wavulana
c.        Mjakazi          wajakazi
d.      Mwenzi          wenzi
e.        Mwanadamu    wanadamu
Mofu
Mofu za idadi
//umoja//---------{m}/-k
-------- {mw}/-i
//wingi//--------- {wa}/-k
---------- {w}/-I
Kanuni ya tatu; Kanuni hii inadai kuwa alomofu moja au zaidi zimo katika mtawanyo mkamilishano ambapo moja ikitokea basi ya pili haitokei. Yambwa na yambiwa haziwezi kutokea katika mazingira yale yale.
Mfano
a.       Baba alinimpigia mimi simu
b.      Sisi tuliwamuona nyinyi
c.       Yeye alimwakuta wao
-          (m)  na  (mu)
-          (wa) na  (w)
Zimo katika mtawanyo mkamilishano au mgawanyo wa kiutowano
 Kanuni ya nne; Umbo moja na zaidi huweza kuwa katika mpishano huru kama maumbo hayo yana maana moja na yametokea katika mazingira yaleyale.
   Mfano
a.       Ngombe badala ya ng’ombe
b.      Khabari badala ya habari
c.       Lafiki badala ya Rafiki
d.      Ntoto badala ya motto
Kanuni ya tano; inadai kuwa maumbo yenye maana tofauti ni Mofimu na maumbo tofauti yenye maana sawa ni alomofu.


     MATATIZO YA KUTENGANISHA MOFU
1.      Tatizo la kwanza ni kukosekana kwa umbo dhahiri la mofu
    Mfano:
a.       θ+chungwa: ma+chungwa
b.      θ+bega    : ma+bega
c.       θ+jiwe    : ma+we
d.      θ+shati   : ma+shati
 Katika mifano hiyo mofimu za umoja ni {θ} na za wingi ni {ma} 
2.      Tatizo la pili ni kukosekana maneno asilia yanayozalisha maneno unde.
    Mfano:
a.       Fupi – fupika –fupisha
b.      Refu - refuka –refusha
c.       Kau  – kauka – kausha
Mifano hiyo ina maneno asilia na maneno unde. Maneno (fupi na refu) ni maneno asilia ya maneno unde fupisha na refusha. Lakini (kau) sio neno asili la neno (kauka na kausha) kwa sababu neno hilo (kau) halikubaliki kwa maneno ya namna hiyo
3.      Tatizo la tatu: ni ugumu wa kutenganisha mofu katika maneno mwambatano.
     Mfano:
a.       Mwanajeshi
b.      Mu-ana-jeshi
c.       Mw-ana-jeshi
d.      Mw-an-a-jeshi
e.       Mw-anajeshi
Maneno mwambatano yanaundwa kwa mzizi zaidi ya mmoja hivyo huwa ni vigumu kubaini mofimu ni zipi na mizizi ni ipi. Hivyo mfano (b) mpaka (e) imekosewa katika kutenganisha mofu. Ni vigumu kutenganisha mofu katika maneno ya mwambatano.

MAKUNDI YA MANENO
 Katika lugha kuna aina mbalimbali za maneno ambazo zina taratibu zake ambazo zinafanya ziwe wazi au zimefungwa hivyo tunaweza kupata makundi mawili.
Makundi ya wazi na Makundi yaliyofungwa. Aina ya maneno katika lugha ambazo unaweza kuyaingiza maneno mapya bila kizuizi.  Mfano; nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi nk.
Makundi yaliyofungwa Mfano; viunganishi kama vile “na, lakini, walakini nk ni maneno ambayo hayaruhusu maneno mapya kuingia kwa namna mbalimbali. Viingizi=Maneno yanayotangulia katika kuunda sentensi. Mfano; Yesu na Maria. Uundaji wa maneno mapya unahusu ubadilishaji wa maneno kuunda maneno mengine.
 Mfano;
a.       uchekeshaji
b.      ucheshi
c.       vichekesho
  Vyote ni nomino za aina moja.  -Unaweza kupata vivumishi kutokana na kivumishi, nomino, kitenzi nk. Unaweza kunyumbua maneno ya aina mbalimbali, hapa tutaanza na unyambuzi wa vitenzi. Kitenzi ni maneno yanayotoa taarifa juu ya tendo linalifanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu. Imefafanuliwa kwa kutilia maanani kama/kwa namna linavyotumika katika sentensi.                        
 AINA ZA VITENZI
i)                                      Kitenzi kikuu mfano; Analala
ii)                                    Kitenzi kisaidizi mfano; Alikuwa analala
iii)                                  Kitenzi kishirikishi mfano; Huyu ni mtoto.
Msingi uliotumika katika kuunda aina za vitenzi ni wa kisintaksia sio kimofolojia. Msingi wa kimofolojia wa uainishaji wa sentensi ni kutazama umbo la kitenzi ambalo linaweza kupatikana katika kamusi.
Mfano; la-la              Kul-a-la              Kuj-a           
Maumbo ya vitenzi. Mizizi yenye sauti au herufi mbili. Mfano; Ol-a, On-a -Jumla ya maneno
Sauti tatu na herufi nne Mfano; Teng-a, Pang-a. Maumbo ya vitenzi yenye sauti tatu na herufi sita Mfano; Shang-a, Chungu-a -Sauti sita na herufi saba
Mfano; Tengam-a
Katika Kiswahili kiuna maneno yamekopwa kutoka katika lugha nyingine mfano, rudi, adabu, hakiki nk
 Maumbo hayo pia hubeba maana fulani ambapo yanaweza kuwa na sifa mojawapo kati ya hizi mbili;
Sifa elekezi, huwa ndani ya mzizi. Kwa kawaida kitenzi hicho huambatana na yambwa nyingine kwa lazima. Mfano; O na a, O- imeruhusu kuandamana na yambwa.
 Si elekezi- Ni mizizi isiyolazimisha kitenzi kuambatana na kipashio kingine.            
 VIAMBISHI NYAMBUZI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
a.                   Kiambishi kitendwa. Hiki huwakilishwa na kiambishi “{-w-}”
b.            Kiambishi kitendeka. Huwa mna umbo la “{-ik-}”, “{-ek-}”
c.             Kiambishi kitendeshi. Huwa na maumbo ya {-ish-},{- esh-}, {-iz-},{- ez-}
d.            Kiambishi kitendea. Huwa na umbo la i/e, {-il- }/{-el-}
e.             Kiambishi kibadilifu (reversive). Huwa na umbo la{- o-}/{-u-}
f.             Kiambishi kifungamanishi (static). Huwa na umbo la am
g.            Kiambishi kishikanishi (contactive). Huwa na umbo la al       
h.            Kiambishi kitenganishi (resprocal). Huwa na umbo la {–an-}
 NB: Hivi ni viambishi tofauti na viambishi vingine tulivyoviona. Mfano; Teng-a. {a} - ni kiambishi kuonyesha dhamira. 
MUUNDO WA MANENO
Neno huundwa na viambishi mbalimbali. Mfano wa maneno kutoka lugha ya Kiswahili itatolewa mfano; vitenzi, nomino na vivumishi.

I. NOMINO
Nomino ni neno linalotaja kitu kitu, kiumbe, hali, dhana na tendo kama vile ua, mti, tausi, mtandao,Ali, uzuri n.k. katika Kiswahili Nomino zina maumbo ya aina nne:
a.          Umbo huru kama vile; Simba, Jeni, Mombasa, baba n.k
b.         Umbo la kiambishi awali na Mzizi kama vile m-zimu ambapo m-ni kiambishi awali na –zimu ni mizi wa neno. Mifano mingine ya aina hiyo ni: mt-tu, ki-kapu, m-sumari, u-zuri, ji-ko, ma-yai n.k
c.          Umbo la Kiambishi awali, Kiambishi tamati na Mzizi, kama vile; ma-vun-o, m-chez-aji.
d.         Umbo la Mzizi na Kiambishi tamati, kama: tuz-o,fund-i.
Katika Kiswahili, kama ilivyo katika lugha za familia ya Kibantu, nomino hujigawa katika makundi yaitwayo ‘ngeli’ kisarufi. Kila nomino ya Kiswahili maskani au makazi yake ni katika ngeli yake. Ngeli ni mgawanyo wa aina mbalimbali za nomino, zaidi kwa msingi wa viambishi awali katika maumbo ya nomino au vilevile kwa msingi wa viambishi vinavyotangulia maneno yanayoambatana na nomino katika sentensi. Viambishi hivi kwenye maneno yanayoambana na nomino katika sentensi hujulikana pia kama “viambishi vya upatanisho wa kisarufi”. Kwa mfano tukio la kukutanisha nomino na kiwakilishi kionyeshi huonyesha waziwazi asili ya nomino kwa kiambishi kama ifuatavyo:
a.        Mtoto huyu
b.       Kikapu hiki
c.        Yai hili
d.       Ubao huu
e.       Mti huu
f.        Nyumba hii
g.       Kucheza huku
h.       Longido hapa
Katika nomino hapo juu (a)-(h) zinaonesha kila moja kupatanishwa kwa kiambishi kilichochorewa kistari pale kinapoambana na kiwakilishi kionnyeshi. Hivi, kundi mojawapo la viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli za nomino katika Kiswahili.
Aidha, kuna matumizi ya nomino na upatanisho wa kisarufi yanayotokana na athari za mifumo ya ngeli ya lugha nyingine za Kibantu kama ifuatavyo:
2. Katoto haka.

II. KITENZI
Kitenzi ni aina ya maneno inayoeleza tendo linalofanywa na nomino (Khamis, 2009:13). Mifano ya vitenzi ni kama vile og-a, li-a, koho-a, sinzi-a, pumu-a n.k. anafafanua kwamba maumbo ya vitenzi kuhusisha mzizi na kiambishi tamati –a ndiyo maumbo asili na ya msingi yanayopatika katika kamusi. 
Kihore (2009:13) anaeleza kuwa kitenzi ni aina ya maneno inayota taarifa juu ya tendo linalofanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu. Mfano ya vitenzi katika Kiswahili ni pik-a, tembe-a, andik-a, som-a, abudu, shukuru, ag-a n.k. anakubaliana na maelezo yaliyotolewa na Khamis (2009) kwa kusema katika mifano hiyo hapo juu kuna vitenzi ambavyo vimeambikwa kiambishi mwishoni na vile ambavyo havijaambikwa. Anasema; kwa kawaida, vitenzi vile vilivyoambikwa ni vya asili ya lugha  wakati vile ambavyo havikuambikwa ni vya asili ya lugha ya kigeni.  Kutokana na maelezo hayo ya Kihore na Khamis (washatajwa), Wesana-Chomi (2013:37) anahitimisha kwa kusema, Mofolojia ya kitenzi katika Kiswahili ni muundo wa Mzizi tenzi pamoja na kiambishi tamati kimoja au zaidi. {MZ + K}. Anatoa mifano ifuatayo:
2. Mzizi                           Kiambishi                     3. Mzizi                       Kiambishi   Kiambishi
·         Pig                               a                                  pig                               an                    a
·         Som                             a                                  som                              esh                   a
·         Let                               a                                  let                                e                      a
·         Chuku                         a                                  chuku                          liw                   a
·         Jeng                             a                                  jeng                             ek                    a

Mifano katika (2) ni vitenzi vya msingi. Kitenzi cha msingi ni muundo wa mzizi tenzi na kiambishi tamati kimoja tu ambacho ni kiishilizi (ishilizi). Mara nyingi kiambishi tamati hiki huwa ni irabu “a”. Mifano katika (3) ni vitenzi vya mnyumbuliko.
Anabainisha zaidi kuwa katika kitenzi cha msingi au kitenzi mnyambuliko huongezwa kiambishi awali kimoja au zaidi na kuunda tungo kama vile:
a.        anasomo                                    a. alinisomesha
b.      wataimba                                    b. nilimsomea
c.       tumecheza                                  c. ilisomwa
d.       hakusoma                                  d. walituimbia
e.       hawataimba                                e. hauimbiki
f.       sijacheza                                      f. aliimbisha
Chanzo: (Chomi, 2013:37)
Katika mifano hiyo, vitenzi hivyo si vitenzi tu bali ni tungo tenzi zenye sifa za kisentensi. Vitenzi hivyo vimebeba viambishi vipatanishi kama vile; a, wa, tu, ni, i, ye- ambavyo vinasababisha tungo tenzi hiyo kuwa na hadhi ya sentensi. Kwa mfano Kihore (2009:14) anasema uambishaji wa viambsihi katika mzizi wa kitenzi huto tungo ambazo ni sentensi kamili kwa kuwa vinahusisha mtendaji wa tendo, wakati tendo lilipotendwa na anayetendewa tendo. Anabainisha vitenzi vyenye sifa ya kuwa sentensi kamili kulingana na uambishaji kama ifuatavyo:
a.        Nilimwona                            ni-li-mw-on-a
b.      Kimeanguka                           ki-me-anguk-a
c.       tunalala                                    tu-na-lal-a                   
d.       wanasafiri                               wa-na-safiri
e.        tuliowaita                               tu-li-o-wa-it-a
f.        hawataondoka                        ha-wa-ta-ondok-a
g.      sijawatazama                           si-ja-wa-tazam-a
Swali. Vitenzi vya lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Kibantu vina sifa ya kuwa sentensi kama sentensi nyingi. Jadili kauli hii.
Miundo ya vitenzi vya Kiswahili
i. Umbo la Mzizi na Kiambishi tamati ishilizi
Kama ilivyoelezwa hapo juu hili ndiyo umbo msingi la vitenzi vya lugha ya Kiswahili. Kwa mfano; som-a, lim-a, to-a. nyw-a, ny-a, f-a, j-a n.k.
ii. Umbo la Mzizi na Viambishi nyambulishi; Kama vile:
a.       Pig-a                pig-an-a, pig-an-ish-a, pig-an-ish-w-a, pig-an-ish-i-w-a
b.      Fung-a             fung-ish-a, fung-ish-an-a, fung-ish-an-ish-a, fung-ish-an-ish-ik-a
Kihore (2009:14) anabainisha kuwa katika kiswahili umbo hili la kitenzi linaweza kuruhusu mfuatano viamshi mpaka vinne (04) kama mifano hiyo inavyoonesha.
iii. Umbo la Kitenzi ni
Umbo hili hujitokeza tu kwenye tunog yakinishi za njeo ya wakati uliopo huwa pia haiandamni na viambishi katika tungo kama ilivyo kwa aina nyingine iliyotangulia. Ni aina ya vitenzi ambavyo hutaja hali ya mtu. Kwa mfano:
a.       Juma ni mwalimu
b.      Asha ni mrembo
III. KIVUMISHI
Kivumishi ni neno linachukuzana na nomino likieleza zaidi sifa yake. Mfano wa vivumishi katika lugha ya Kiswahili ni kama vile; kubwa, tamu, chungu, safi, chafu n.k
       Umbo la Vivumishi
Kivumishi kina maumbo mawili ambayo ni:
1.      Umbo Huru; kama vile dogo, pana, gumu, zuri n.k
2.      Umbo lililonyambulishwa; kama vile: nyenyeke-vu (nyenyekea), stahimili-vu (stahimili) n.k. vivumishi vyenye umbo lililonyambulishwa ni vile vilivyotokana na aina nyingine ya maneno.
Kwa kawaida katika tungo, vivumishi hasa vya asili ya lugha ya Kiswahili huwa vinaambishwa viambishi vya nomino vinavyoandamana nazo. Kwa mfano:
a.       Mbuyu m-kubwa
b.      Mibuyu mi-kubwa
c.       Kikapu ki-dogo
d.      Mhogo m-chungu
Viambishi hivi hujulikana kama viambishi vya upatanisho wa kisarufi. Kwa kawaida viambishi vya upatanishi huwa haviambishwa kwa vivumisho vilivyokopwa kutoka lugha nyingine kama mifano ifuatayo inavyoonesha:
a.       Watu sita na siyo (watu wasita*)
b.      Vikombe saba siyo (vikombe visaba*)
c.       Mfuko laini siyo (mfuko mlaini*)
d.      Msichana jamili siyo (msichana mjamili*)
Katika mifano hiyo nomino zinazojitokeza mwanzoni mwa tungo hufuatwa na vivumishi ambavyo vimekopwa kutoka lugha ya Kiarabu.
IV. KIELEZI
Ni aina ya maneno yanayoeleza zaidi kuhusu kitenzi kinachoambatana nacho katika tungo. Mfano wa vielezi katika Kiswahili ni vizuri, polepole, sana, mno n.k.
Maumbo ya Vielezi
Kimofolojia vielezi hugawanyika katika makundi matatu
1.   Kundi la umbo huru (Vielezi Halisi) k.m sana, mno, upesi, harka n.k
2.   Kundi la umbo lilioambikwa (Vielezi Ambikwa) kama vile vi-zuri, vye-ma, ki-dogo n.k
3.   Kundi la Umbo radidi kama vile; kimyakimya, polepole, chinichini n.k
Katika tungo, vielezi huwa haviambishwi viambishi vya upatanishi wa kisarufi kama ilivyo kuhusiana na vivumishi vilivyojadiliwa hapo juu. Aidha, katika tungo vielezi tofauti huweza kuandamana na kitenzi kama mfano ufuatao unavyoonesha:
a.       Anatembea haraka sana
b.      Tumekula vizuri kabisa
c.       Wanaongea polepole mno
d.      Mmeshindwa vibaya kweli kweli

   

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Kitabu : Mofolojia ya kiswahili

Matini hii ya Mofolojia ya Kiswahili sanifu kwa sekondari na vyuo inachukua nafasi yake katika Mofolojia ya Kiswahili ambacho bado haijachapishwa kuwa kitabu rasmi kipo katika marekebisho kuanzia mwaka 2017. Kwa hakika matini hii ni moja ya matini ambayo huweza kukidhi mahtaji ya kufundishia somo la Kiswahili katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Matini hii imetayarishwa katika muktadha wa kukidhi Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Matini hii ni tofauti na mtini nyingine za awali kwa namna kadhaa. Kwanza matini hii imeelezea fasili ya mofolojia kama taaluma nyingine za isimu ya lugha katika Kiswahili. Pili dhana kadha wa kadha ambazo zilikuwa zinachanganya au zina maelezo pungufu katika matini za awali zimetazamwa upya na kupewa maelezo ya kina na uwazi zaidi hasa dhana ya mofu na mofimu zinavyochanganywa na wataalamu mbalimbali. Pia hali hii inajidhirisha katika alomofu, dhana ya mofofonolojia, unyambuaji, uambishaji na uundaji wa maneno. Dhana ya sarufi maumbo amba...

SHAIRI DUNIA MTI MKAVU

.                           DUNIA MTI MKAVU Hekima na busara ni sawa na ujinga na upumbavu Furaha na kicheko ni sawa na huzuni na kilio Sehemu yenye mwanga ni s awa na sehemu yenye giza Ukitenda wema unaweza kulipizwa kwa mateke Ukitenda mabaya unaweza kulipizwa kwa wema Binadamu anamdharau panzi kwa sababu ni mdudu Lakini tambueni panzi atakuja kuwa na thamani kama ng'ombe Mwenzako akimwaga ugali mwaga unga Na mwenzako akimwaga mboga mwaga mafuta Mwanadamu kama hujui ndoa ni mkono karibu na goli Na firimbi imelia golini hamna mtu Lakini goli upana futi moja viatu vimechanika na mpira ni tofari Uwanja kijiji ndani ya nyumba Washangiliaji na wazomeaji wengi sana Maswali mengi kama hayo manung'uniko mengi kama hayo Matatizo mengi kama hayo sasa Yanaonekana ingawa zamani hayakuwako Lakini haya yote yataisha Binadamu wenzangu tambueni dunia hii imegeuka. Kushoto kumekuwa kulia na kulia kumekuwa kushoto Dunia imegeuka ku...