DHANA YA MOFU, MOFIMU NA ALOMOFU
Dhana ya mofu
Mgullu, (1999)
anasema kuwa dhana za mofu, alomofimu na mofimu ndizo ambazo hutumiwa sana kwa
uchambuzi wa kiisimu hususani katika kiwango cha mofolojia. Istilah hizi zote
zimetoholewa kutoka istilahi za kingereza, yaani
a.
Mofu kutoka morph.
b.
Alomofu
kutoka allomorph.
c.
Mofimu kutoka morpheme
Inafaa dhana
hizi tatu zielezwe vizuri kwa sababu ni dhana muhimu sana katika isimu. Lakini
kwa bahati mbaya dhana hizi huchanganywa changanywa sana wakati wa kuzitumia
kiasi ambacho kimefanya dhana hizi zionekane kuwa niza kutatanisha siyo katika
uchambuzi wa lugha ya Kiswahili tu bali pia hata lugha ya kiingereza ambako
zimetokea. Tunasisitiza hapa kuwa dhana hizi zinafaa zielezwe kwa makini na kwa
uangalifu wa kutosha ili zisipotoshwe kama ambavyo watu wengine wamekua
wakizipotosha.
Dhana ya mofu
Kama
tulivyoeleza apo juu kwa mofu ni istilahi ambayo imetoholewa kutoka istilah
morph kutoka lugha ya kiingereza Nida (1949) anaeleza kuwa, Mofu ni umbo la
neno ambalo huwakilisha mofimu ambalo hudhihirika kifonolojia na kiothografia.
Mofimu ambazo ni elementi dhahania huwakilishwa na mofu ambazo hudhihirika ama
kifonolojia zikiwa ni sauti za kutamkwa za kutamkwa au kiothografia zikiwa ni
alama za kuandikwa. TUKI (1990) wanasemaje kuwa, Mofu ni kipashio cha kimofolojia
kiwakilishacho mofimu.
Platt (1985)
naye anaeleza ya kuwa mofu ni kipashio kidogo kabisa chenye maana kabisa katika
lugha. Mofu haiwezi kugawanywa katika sehemu ndogo zaidi bila kuharibu maana
yake. Mofu huwakilisha maana za kileksika na zile za kisarufi.
Fasili hizi tatu
zinaeleza mambo ya msingi kabisa kuhusu sifa muhimu zinazopambanua dhana ya
mofu sifa hizi ni pamoja na;
Mofu ni sehemu halisi ya neno
Kinachoelezewa
hapa ni kuwa mofu ni maumbo halisi ya
maneno ambayo hutamkwa na watu wanapozungumzoa au kuandikwa wakati
wanapoyaandika maneno. Kwa hiyo mofu ni umbo halisi ambalo tunaweza kulisikia
linapotamkwa na kuliona linapokuwa limeandikwa.
Mofu hudhihirika kifonolojia na kiothografia
Kwa kuwa mofu ni
ubo halisi la neno, basi mofu mbalimbali hudhihirika kifonolojia zinapotamkwa
na pia kimaandishi zinapoandikwa.
Mofu huiwakilisha maana
Hapa
tunasiisitiza kuwa mofu huwakilisha maana fulani. Kwa hiyo katika neno lolote
katika mofu zilizopo katika neno. Hii inatufanya tuelewe kama kila neno huwa na maana fulani basi
maaana hiyo lazima itakuwa imewakilishwa na mofu fulani. Hii ina maana kuwa
hakuna neno lolote katika lugha yoyote ambalo linaweza kuwa ni neno lenye maana
bila kuwa na mofu angalau moja.
AINA ZA MOFU
Kwa mjibu wa Mngullu (1999) anasema kuwa mofu
huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili:
·
Kigezo cha maana zinazowakilishwa na mofu;
·
Kigezo cha mofolojia ya mofu.
Tunapotumia kigezo cha maana zinazowakilishwa
na mofu, tunapata aina tatu za mofu, yaani:
a.
Mofu huru
b.
Mofu funge
c.
Mofu tata
Kwa upande mwingine tunapotumia kigezo cha
mofolojia au maumbo ya mofu zenyewe tunapata aina mbili za mofu, yaani:
a.
Mofu changamano
b.
Mofu kapa
Kwa mantiki hii tunazo aina tano za mofu
ambazo ni:
a.
Mofu huru
b.
Mofu funge
c.
Mofu tata
d.
Mofu-changamano
Mofu Huru
Weber (1985) anasema kuwa mofu huru ni zile mofu ambazo
zinaweza kukaa peke yao kama maneno kamili.
Mofu huru ni zile mofu ambazo zinaweza kukaa
peke yake kama maneno kamili yenye maana inayoweza kueleweka bila kusaidiwa na
mofu nyingine. Aghalabu, mifano mingi ya mofu huru hupatikana kutoka kwenye
vipashio vya lugha, kama ifuatavyo:
a.
Nomino: {baba}, {kuku}, {sungura},
{ndege}, {dada}, {paka}, nk.
b.
Vivumishi: {safi}, {baya}, {dhaifu}, {zuri}, {imara},
{hodari}, nk.
c.
Viwakilishi:{mimi}, {sisi}, {wewe}, {ninyi}, {yeye),
{wao}, nk.
d.
Vielezi: {upesi}, {haraka}, {sana},
{leo}, {jana}, {juzi}, nk.
e.
Vitenzi: {tafiti}, {samehe}, {arifu}, {sali}, {jibu}, {badili}, nk.
f.
Vihusishi: {ya}, {juu}, {mbele}, {kwa}, nk.
g.
Viunganishi:{na},{halafu}, {bado}, {ila}, {aidha},{pia},
nk.
Kwa mujibu wa mifano hii inadhihirika kwamba
Kiswahili kinazo mofu huru nyingi ambazo zimo katika aina zote za vipashio vya
lugha. Hivyo, mofu huru ni mofu ambazo zinaweza kukaa peke yake kama maneno
kamili yanayoeleweka bila kusaidiwa na viambishi.
Mofu funge au Mofu tegemezi
Richards et al. (1985) wanaeleza ya kuwa mofu funge ni
kipashio cha kiisimu ambacho huwa hakikai peke yake bali ni lazima kiandamane
na mofu nyingine.
Hartman (1972) naye ana mawazo yanayofanana sana nay ale ya Richards
et.al (1985). Hartman anasema kuwa mofu funge ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa
peke yake kama neno kamili lililo na maana yake bainifu, bali (daima) hutumiwa
kama kiambishi tu kinachoambatana na mzizi au viambishi vingine ili kukamilisha
neno.
Mofu funge au Mofu
tegemezi ni mofu ambayo haiwezi kutumiwa peke yake kama neno lililo na
maana yake kamili; aghalabu mofu funge hutumiwa kama kiambishi tu
kinachoambatanishwa na mzizi au viambishi vingine ili kulikamilisha neno
husika. Mofu funge ina sifa zake ambazo ni pamoja na:
(a)
Mofu funge haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili.
(b)
Mofu funge ni lazima iambatanishwe na angalau mafu
nyingine moja ndipo tupate neno kamili.
Kutokana na sifa hii ndiyo mdiyo maana wanaisimu wengine huziita
mofu hizi kuwa ni mofu
tegemezi ambayo ina maana sawa na mofu funge
Mfano:
Idadi ya
Umoja Idadi ya Uwingi
a.
m-toto (m) wa-toto (wa)
b.
ki-su
(ki) vi-su (vi)
c.
m-ti
(m) mi-ti (mi)
Ukumbwa wa
Nomino Udogo wa Nomino
a.
ji-tu
(ji) ki-ji-tu (ki)
b.
ji-su
(ji) ki-ji-su (ki)
Maana za mofu funge hutegemea sana muktadha
wa mofu funge husika. Mofu funge ikiondolewa kwenye muktadha wake hukosa maana
na ni vigumu kujua maana yake bila kuiweka katika muktadha wa neno. Mofu funge
inaponing’inizwa peke yake haituwezeshi hata kidogo kujua maana yake. Umbo moja
linaweza kuwa na maana nyingi kwa mujibu wa miktadha ambamo imeambatanishwa
katika mzizi wa neno.
Aghalabu, mofu funge ni sawa na viambishi vya
mizizi mbalimbali katika neno. Hii ina maana kwamba viambishi vilivyo vingi
katika lugha huwa ni mofu funge. Tunasema viambishi vingi kwa sababu si
viambishi vyote ambavyo huundwa kwa mofu funge. Vipo viambishi vingine ambavyo
huundwa kwa mofu huru. Baadhi ya mizizi ya maneno pia huwa ni ya mofu funge kwa
sababu mizizi hiyo huwa haiwezi kukaa peke yake ikawa neno kamili. Mifano
mizuri ya mizizi ya maneno ya Kiswahili ambayo huundwa kwa mofu funge ni ile ya
vitenzi vya silabi moja moja, kama ifuatavyo kwa mfano:
Mofu
funge Neno Mofu
funge Neno
a.
{-l-) kula {-p-} mpe
b.
{-j-} kuja {-ny-} kunya
c.
{-f-} kufa {-nyw-} kunywa
d.
{a} + {me} + {m} + {nyw} + {esh} + {a} amemnywesha
Mizizi ya vitenzi hivi ni mizizi ya
mofu-funge kwa sababu haiwezi kutumiwa peke yake kama neno na, pia maana zao
huwa hazijitokezi mpaka mizizi iwekewe viambishi.
(iii) Mofu Tata
Mofu tata ni mofu ambazo huwa na maana zaidi
ya moja au kuanzia mbili na kuendelea.
Mfano:
Saidi
alimpigia Mbaraka mpira.
Sentensi hii ni tata kwa sababu ina maana
zaidi ya moja. Utata wa sentensi hii haupo kwenye muundo wake wa kisarufi, bali
upo katika kitenzi alimpigia. Kitenzi hiki kina mofu sita, yaani:
{a-} + {-li-} + {-m-} + {-pig-} + {-i-} + {-a}
1 2 3 4 5 6
Kati ya mofu hizi zote sita, mofu ya tano
{-i-} ndiyo yenye utata. Mofu {i} ni mofu ya kutendea kwa sababu tukisema: ‘Saidi
alimpigia Mbaraka mpira’, maana zinazoweza kueleweka na wasikilizaji ni nne:
a.
Saidi aliupiga mpira kwa niaba ya Mbaraka; yaani Mbaraka
ndiye aliyetakiwa aupige mpira ule, lakini kwa sababu ambazo hazikuelezwa,
badala ya Mbaraka kuupiga mpira ule, Saidi akaupiga.
b.
Saidi aliupiga mpira kuelekea kwa Mbaraka; yaani Saidi na
Mbaraka walikuwa wakicheza mpira. Ikapatikana fursa, Saidi akaupiga mpira ule
kuelekea kwa Mbaraka. Kwa hiyo, hapa tunazungumzia mwelekeo wa mpira.
c.
Saidi alimpiga Mbaraka kwa kuutumia mpira; yaani, Saidi
anautumia mpira kama ala (silaha) ya kumpigia Mbaraka.
d.
Saidi alimpiga Mbaraka kwa sababu ya mpira; yaani hapa,
mpira ndio sababu kubwa ya Saidi ya kumpiga Mbaraka. Tuseme labda Saidi alikuwa
na mpira wake, halafu Mbaraka akauchukuwa kuuchezea na kwa bahati mbaya
akaupoteza. Saidi anapogundua kwamba Mbaraka ameupoteza mpira wake, basi ndipo
akampiga.
Kwa maelezo hayo, ni wazi kwamba sentensi
yetu ina utata kwa kuwa inatupatia maana tofauti tofauti zipatazo n’ne ambazo
zimesababishwa na mofu {-i-} ya kutendea.
(iv) Mofu Changamani
Mofu changamani ni mofu ambazo huundwa kwa
kuweka pamoja angalau mofu-sahili mbili au mofu funge na mofu sahili
yakafanyiza neno lenye kuleta maana kamili, kwa mfano:
Mofu sahili +
Mofu sahili
a.
{askari} + {kanzu} = askari
kanzu.
b.
{gari} + {moshi} = gari moshi.
c.
{paka} + {shume} = paka shume.
d.
{m’mbwa} + {mwitu} = m’mbwa
mwitu.
e.
{fundi} + {chuma} = fundi chuma
Mofu
funge + Mofu huru
a.
{mw} +
{-ana}+ {nchi} = mwananchi.
b.
{ki} + {-on-} + {a} + {mbali}= kiona mbali.
c.
{mw} +
{-ana}+ {hewa
}= mwanahewa. n.k
(v) Mofu Kapa
Mofu kapa ni mofu za pekee ambazo hazina
umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno,
lakini athari zinazotokana na hiyo mofu kapa husika hueleweka. Ingawa mofu hizi
huwa hatuzioni wala kuzitamka au kuziandika, lakini maana zake tunazipata.
Tukichunguza ruwaza ya viambishi awali vya umoja na wingi katika lugha ya
Kiswahili, tunaweza kuzigawa nomino za Kiswahili katika makundi makuu man’ne,
yaani:
Nomino zilizo na viambishi
bayana vya idadi ya umoja na
uwingi:
Mfano:
Umoja Wingi
a.
m - tu wa - tu
b.
m - toto wa - toto
c.
m - ti mi – ti
Nomino zilizo na kiambishi
awali cha umoja tu, cha wingi hakipo, kwa hivyo, ni kapa (φ)
Mfano:
Umoja Wingi
a.
u -
kuta φ - kuta
b.
u - funguo φ - funguo
c.
u – kucha
φ – kucha.
Nomino zilizo na kiambishi cha
wingi tu, cha umoja hakipo; kwa hivyo, ni kapa (φ)
Mfano:
Uoja Wingi
a.
φ –
kasha ma – kasha.
b.
φ –
debe ma – debe.
c.
Φ –
jembe ma – jembe.
Nomino zisizo na kiambishi
awali cha umoja wala cha wingi
Mfano:
Umoja Wingi
a.
θ -
mama θ - mama.
b.
θ -
ng’ombe
θ - ng’ombe.
c.
θ -
baba
θ -
baba.
d.
θ -
kaka θ - kaka.
e.
θ -
dada
θ - dada.
f.
θ -
mbuzi
θ - mbuzi.
g.
θ -
ngamia
θ - ngamia.
h.
θ -
kondoo θ - kondoo.
i.
θ -
tembo θ - tembo.
j.
θ -
sungura θ - sungura.
k.
θ -
nguruwe
θ - nguruwe
(e) Sherehe
kuhusu Mofu kapa
Katika kuonyesha mofu kapa tutatoa sherehe
kuhusu makundi haya Katika makundi hayo hapo juu nomino zina kiambishi awali
cha umoja tu, wakati cha wingi hakipo. Kinachotokea hapa ni kwamba ukisema
ukucha watu wanaelewa kuwa ni ukucha mmoja tu. Lakini ukisema kucha, watu wataelewa kuwa ni kucha nyingi. Na hali hii ndivyo ilivyo kwa maneno ufunguo ǂ funguo; ukuta ǂ kuta, nk. inajulikana kuwa ni ufunguo mmoja tu na akisema funguo,
ni kwa maana ya wingi; lakini umbo lenyewe linaloileta hiyo maana ya wingi
halionekani bayana katika neno.
Ili
kuyaeleza haya maumbo ambayo hayapo lakini maana zinazowakilishwana maumbo hayo
zipo, Wanaisimu wamekubaliana kuyaita maumbo haya kapa, yaani mofu ambazo
hazipo. Mofu hizi ni dhahania tu katika akili zetu
kwa kufahamu tu kwamba maana fulani haiwezi kuja tu yenyewe lazima iletwe na
mofu fulani. Kwa hivyo, hata kama mofu hiyo haionekani, lakini ipo; ni
mofu-kapa.
Kwa mfano, katika matamshi ya maneno: kasha,
debe, jembe, umoja na uwingi wake hudhihirishwa kama ifuatavyo:
Umoja Uwingi
a.
kasha makasha
b.
debe madebe
c.
jembe majembe
Katika nomino hizi mofu ya uwingi ni
mofu {ma} lakina
mofu ya umoja ni mofu kapa, yaani haipo na huoneshwa kwa alama {Φ}.
Kwa mantiki hiyo, mofu za maneno haya ni kama
ifuatavyo:
Umoja Uwingi
a.
{θ } +
kasha {ma} + {kasha}
b.
{ θ } +
debe {ma} + {debe}
c.
{θ}+jembe {ma}+{jembe}
Dhana ya mofimu
Ingawa katika
kazi hii kuieleza dhana ya mofu lakini historia inaonyesha kuwa histilahi ya
mofimu ndiyo iliyoanza kutumiwa kabla istilahi ya mofu. kwa mujibu wa
crystal (1971) wakati
wa sarufi mapokeo
( traditional grammar)
uchambuzi wa kiisimu. katika
kipindi hiki sentensi iligawanywa ( segmented)
katika vipashio vidogo vidogo
kama vile vishazi , virai na hatimaye neno. lakini baadaye katika karne za 18
na 19 ilibainika kuwa palikuwa na haja ya kwenda chini zaidi yaneno. wakati huu ndipo istilahi
ya mofimu ilipoanza
kutumika .mofu ilianza
kutumika baadaye zaidi katika
karne ya 20 hasa baada ya kuasisiwa
kwa sarufi zalishi. Dhana ya mofimu ina sura kuu mbili zinazo tofautiana
sana. sura hizo zinalingana na vipindi vikuu viwili ambamo dhana hii
ilitumika,yaani:
a.
Dhana
ya mofimu ya kusisiwa kwa sarufi zalishi.
b.
Dhana
ya mofimu baada ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi.
c.
Dhana
ya mofimu kabla ya sarufi zalishi
Wanaisimu
walipoona umuhimu wa kuwa na kipashio kidogo zaidi ya neno katika uchambuzi
mara walibuni na kuanza kuitumia dhana ya mofimu. Badala ya uchambuzi kuishia
kwenye neno tu, uchambuzi ukawa unaendelea hadi kwenye kiwango cha mofimu. kwa
mfano sentensi kama :
“Tumaini anakata
miti” Ingechambuliwa kama ifuatavyo :
Uchambuzi kabla
ya sarufi zalishi
Tumaini anakata miti
Uchambuzi baada ya kuasisiwa
sarufi zalishi
Tumaini anakata miti
Katika uchambuzi
wa awali sentensi imegawanywa katika sehemu kuu mbili yaani:
1. kiima
(Tumaini) 2.kiarifu (alikata miti) kiima
kina nomino moja (Tumaini) na kiarifu
kina kitenzi na nomino (miti) sentensi ni mfululizo wa maneno matatu. katika
uchambuzi wa baadaye sentensi imegawanywa katika: kiima na kiarifu, kiima kina
nomino moja (Tumaini), kiarifu kina kitenzi (alikata) na nomino (miti), Nomino
Tumaini ina mofimu moja tu (Tumaini), kitenzi alikata kina mofimu nne ({a}+{ li
} +{ kat} +{a}, Nomino miti ina mofimu mbili (mi) + (ti) Sentensi ni mfululizo
wa mofimu saba (7)
Dhana ya mofimu
katika kipindi cha kabla ya sarufi zalishi ni sawa na dhana ya mofu
tulivyoieleza hapo juu katika sehemu ya mofu. Yale yote tuliyoyasema kuieleza
mofu ndiyo ambayo tungeweza kuyatumia hapa kuieleza dhana ya mofimu kabla ya
sarufi zalishi. Miongoni mwa wale wanaoitazama dhana ya mofimu kwa jicho hili
la awali ni watu kama Crysstal (1971), Mohamed (1986), Richards et al, (1985),
Kayuza (1988) na Maarealle (1971), Crystal (1971), kwa mfano, anasema kuwa:
Mofimu ni
kipashio kidogo kabisa katika lugha chenye maana zaidi ya hayo, maana hiyo
hutofautiana na zile za mofimu zingine katika lugha hiyo. Mambo mawili yanabainika
hapa. Kwanza ni kuwa ukiongeza au kupunguza mofimu kutoka tamko fulani, bila
shaka maana ya tamko itabadilika.
Crystal (1971)
anaendelea kusema: Kwa hiyo mofimu inazo sifa kadhaa zinazoibainisha, na tatu
kati ya sifa hizo ni muhimu. Kwanza, mofimu ni kipashio chenye umbo halisi.
Mofimu ina umbo lake la kifonetiki. Pili, mofimu huwa na maana. tatu, kila
mofimu huwa na nafasi yake ya kisintaksia katika (kushirikiana na vipashio
vingine) Kuunda vipashio vikubwa zaidi.
Maelezo ya
mofimu anayoyatoa Crystal yanaafikiana nay ale tuliyoyatooa kuhusu mofu katika
sehemu inayotangulia. Utadhani mofu ni sawa na mofimu. Marealle (1978) naye
hatofautiani na Crystal (1971) katika kuifafanua mofimu. Yeye anasema: Mofimu
ni kipashio kidogo kabisa cha kisarufi kilicho na maana. Marealle anatoa mifano
ya mofimu katika maneno yafuatayo ya Kiswahili
A-na-tembea
(mofimu4) 2. A-na-kimbi-a (mofimu 4)
Marealle sawa na
Cystal (1971) anasema kuwa mofimu ni maumbo madogo kabisa ya maneno yenye
maana. Kumbuka kuwa maelezo haya ni sawa na maelezo yetu tuliyoyatoa kuhusu
mofu. Mohammed (1986) naye ana mawazo sawa na Crystal na marealle. yeye anasema
kuwa: Hivyo basi, mofimu ni kijineno au sehemu ndogo ya tamko iletayo maana
kamili ya kisarufi.
Mohammed (1986)
anatoa mfano wa neno anapika. Analigawa neno hili katika vile anavyoviita
vijineno (mofimu) vifuatavyo: a-na-pik-a. Tunaona hapa kuwa dhana ni ile ile ya
sehemu ndogo kabisa ya neno yenye maana. Hata hivyo, maelezo ya Mohamed
yanaweza kuleta neno yenye maana. Hata hivyo, maelezo ya Mohammed yanaweza
kuleta utata. Kwa mfano kuna uhalali gani wa kuziita mofimu kuwa ni vijineno?
je (a) ni kijineno? maana ya neno na kijineno ni nini hapa? pia kuna utata
anaposema kuwa mofimu huleta maana kamili ya kisarufi. Maana zinazoletwa na mofimu
ni za aina mbili, ama za kileksika au za kisarufi. Hatuelewi ni kwa nini
mohammed ameibana fasili yake katika maana za kisarufi tu. Hata hivyo, mfano
wake unatusaidia kujua anachotaka kueleza. Kaayuza (1988) naye yumo katika
kundi lili hili. Yeye anasema kuwa:
Mofimu ndiyo
ngazi ya mwisho ya maumbo. Mofimu ni tamko dogo lenye maana ya kisarufi. kwa
mfano:
Sentensi: Juma a-
na- lim-a shamba
Mofimu: 1
2 3 4
5 6
Ingawa maelezo
yake yana upungufu, lakini mfano wake umetusaidia kuelewa kile kilicho akilini
mwake. TUKI (1990) nao wametumbukia katika mtego huu huu. Wao wanasema:
Mofimu ni
kipashio kidogo kabisa amilifu katika maumbo ya maneno.
Kama
tulivyokwisha kusema, maelezo haya yote ni sawa kabisa na yale tuliyoyatoa
kuhusu mofu. Hawa wanaiona mofimu kuwa ina maana sawa na mofu. tunachoweza
kusema ni kuwa maelezo haya yanaiona mofimu kama kipashio alisi cha neno
kilicho na umbo lake la kifonetiki (wakati maelelezo yanaiona mofimu kuwa ina
maana. Ni maelezo yaiyotumiwa kabla ya kuundwa kwa dhana ya mofu. Baada ya
kuundwa kwa dhana ya mofu maelelzo haya ya mofimu kama kipashio chenye maana
yalihamishiwa kwenye mofu a mofimu ikapewa maana mpya.
Kilicho bayana
ni kuwa kama wakati wa sasa ambapo tunazo istilahizote mbili, yaani mofu na
mofimu, tutaieleza mofimu kama kipashiop kidogo kabisa cha neno chenye maana.
je mofu tutaieleza kuwa ni nini? hufanya dhana za mofu na mofimu zionekane kama
zinafanana, au zinatatanisha.
Dhana ya mofimu baada ya kuasisiwa kwa sarufi
zalishi
Baada ya kuasisiwa
kwa sarufi zalishi katika karne ya 220, dhana muhimu mbili ziliingizwa katika
uchambuzi wa mofolojia ya lugha. Dhana hizo ni mofu na alomofu. Dhana ya mofu
imeelezwa hapo juu na hivyo ndivyo inavyopaswa ieleweke hadi leo. dhana ya
alomofu itaelezwa baadaye. Maana iliyokuwa imepewa mofimu, kama kipashio kidogo
kabisa cha lugha kinachobeba au kusitiri maana. (rejea sehemu ya mofu). Sasa
mofimu ikapewa maana mpya. Fasili mojawapo inayotoa hii maana mpya ya mofimu ni
ile ya Hartman (1972) ambaye anasema
kuwa: Mofimu ni kipashio dhahania cha
umbo fulani ambacho kinaweza kuwakilishwa na mofu tofauti tofauti katika
mazingira anuwai. mofimu ya wingi katika lugha ya kiingereza, kwa mfano, huwakilishwa na mofu /s/, /z/, /iz/ na kadhalika.
Lightner (1975)
naye anaeleza ya kuwa: Kwa kweli mofu imo katika upande wa utendaji lakini
mofimu ni dhana ya kidhahania iliyomko akilini mwa watu na ambayo ni sehemu ya
umilisi wa lugha wa kila mtu. Mofimu ni tafsri ambayo mtu huifanya akilini
mwake kuhusu maana ambayo husetiriwa kwenye mofu.
Fasili hizi
mbili zimepiga hatua kubwa kwa sababu zimefaulu kutofautisha dhana ya mofu na
mofimu. Fasili hizi zina mambo muhimu tunayoyajadili hapa chini.
Mofimu ni kitu dhahania
Hapa tunapewa
ile tofauti ya msingi kuwa wakati ambapo mofu ni sehemu halisi ambazo huwa
tunazitamka au kuziandika tunapoandika maneno lakini maana ambazo huwakilishwa
na mofu hizo ambazo ndizo tunazoziita mofiu bhuwa ni dhahania kwa sababuy maana
hizo huwa hazitamkwa wala kuandikwa. Maana hizo huwa akilini mwa watu. Hapa
kuna tofauti kati ya maana (mofimu) na namna ya kuziwakilisha maana mofimu
(maana) ya wingi katika ugha ya
kiingereza huwakilishwa na maumbo mbalimbali kama /s/, /z/, /iz/, na kadhalika.
Tungeweza kuendeleza hapa kuwa hata katika lugha ya Kiswahili mofimu ya wingi
huwakilishwa na mofu kadhaa kutegemea aina ya nomino inayowekewa wingi. Kwa
mfano, kuna:
a.
Mofu
{wa} katika nomino kama {wa} + toto, {wa} + tu, {wa} + alimu, {wa}+ ungwana,
b.
Mofu
{mi} katika nomino kama {mi} + kono, {mi}+ti+chungwa, {mi}+tume, {mi}+jusi,
c.
Mofu
{ma} katika nomino kama {ma} + cho, {ma} +we, {ma} +no (meno), {ma}+iko (meko),
{ma} +jemadari, {ma} +jambazi, n.k.
d.
Mofu {vi} katika nomino kama {vi}+ atu, {vi} +ti,
{vi} +ti {vi} +tu, {vi} +azi, {vi}
+tanda, {vi} +ongozi, {vi}+ jana, {vi}+pofu,
e.
Mofu
{Ɵ}/ {Kapa} katika nomino kama Ɵkuta, Ɵkucha, Ɵfunguo, Ɵpawa, Ɵ pande, Ɵkuni,
n.k.
Kwa hiyo hii
mifano inaonyesha kuwa, maana (mofimu) ile ile ya wingi inaweza kuwakilishwa na
maumbo {wa}, {mi}, {ma}, {v}, na {Ɵ}.
Maumbo haya yote
yanapotumika katika mazingira yanayofaa huwa yamesetiri ile maana ya wingi. Kwa
Mantiki hiyo mofimu si sehemu iliyopo kwenye neno. Mofimu haziwezi kuhesabika
kwani si vitu halisi ni vitu dhahania. Ni sawa na mtu anapozungumzia maneno na
maana zake. Neno huonekana likatamkwa na kuandikwa. Neno ni sehemu ya utendaji
(performance) na neno lipo upande mmoja na mofu. Lakini maana za maneno ni
dhahania, zipo akilini mwa watu. Maana za maneno huwa hazitamkwi wala kuandikwa
na awatu. Lakini maana hizo huwa akilini mwa watu wanaozungumza na kusikiliza
nah ii ndiyo maana watu hawa huelewana. Maana za maneno zipo upande mmoja na
maana za mofu ambazo tunaziita mofimu. waandishi kama marealle (1978) na Kayuza
(1988) wanafanya makosa makubwa wanapodhani kuwa mofimu ni maumbo ya maneno
yenye maana ambayo tunaweza kuyahesabu. marealle (1978), kwa mfano, anasema
kuwa neno anakimbia lina mofimu nne na anazionyesha:
a+ {na} +
{kimbi} + {a}
1 2 3 4
Haya si maelezo
sahihi. Kayuza (1988) naye anasema kuwa sentensi “Juma analima shamba” ina
mofimu sita na anazionyesha.
(Juma) + (a) + (na) + (lim) + (a) + (shamba)
1 2 3
4 5 6
Mtazamo huu pia
si sahihi. Ama kwa hakika, hizi zote wanazoziita mofimu ni mofu na mofimu ni
maana zilizomo kwenye mofu hizo. maana (mofimu) zilizopo katika sentensi “Juma
analima shamba” ni hizi zifuatazo.
MOFU MOFIMU
1.
{Juma} (1) Mtu,
(2) Idadi: mmoja, (3) Jinsia: mwanaume
2.
{a}
(1) Kipatanishi, (2) Nafsi ya tatu, (3) Idadi: Mmoja
3.
{na} (1) Njeo: sasa, (2) Hali: Kuendelea
4.
{lim} (1) Mzizi wa kitenzi
5.
{a} (1) Kiambishi tamati, (2) Kauli ya kutenda, (3) Yakinishi
6.
.{Ɵ}
(kapa) (1) Idadi ya umoja
7.
{Shamba} (1) Mzizi wa nomino
(2) Ardhi kubwa kuliko inayolimwa kupanda maua.
Kwa ufupi
tunaona mofimu (maana) mbalimbali tunazozipata kutokana na mofu saba kuwa ni
kumi na tano (15). Huu ni uthibitisho mwingine kuwa yale ambayo humjia mtu
akilini anaposikia tamko fulani, yaani mofimu za mofu ni, mengi. Ingawa mofu
zipo saba tu lakini mofimu ni kumi na tano. Mofimu hapa si maumbo ya maneno
bali ni maana tunazozichuja akilini mwetu. Tunapenda tusisitize hapa kuwa tangu
dhana ya mofu ilipoanzishwa baada ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi dhana ya mofu
imepewa fasili iliyokuwa ya mofimu na dhana ya mofimu ikapewa fasili mpya. kwa
sasa mofu ndiyo inayopewa maana ya:
Kipashio kidoo
kabisa cha kimofolojia kinachosetiri maana. Kipashio hiki ni halisi na
hudhihirika kifonetiki na kiothografia.
Nayo mofimu kwa
sasa hupewa ile maana ya dhana ya kidhahania ambayo ni maana ambayo/zo
huwakilishwa au kusetiriwa katika mofu. Tumetumia muda mrefu kuieleza hii dhana
ya mofimu kwa sababu ndiyo kwenye matatizo zaidi kwa sababu mara nyingi huwa
inachanganywa na mofu kiasi kuwa mtu atashawishika kudhani kuwa mofu (umbo) ni
sawa na mofimu (maana). Labda wakati mwingine makosa haya yanatokana na watu
wengine kutokujua kuwa maana ya mofimu imebadilika sana.
Hivyo tunaweza kusema kuwa kabla ya kuasisiwa kwa sarufi zalishi dhana ya mofimu ilichua maana ya mofu kama ilivyojadiliwa katika sehemu iliyotangulia hapo juu. Lakini baada ya kuasisiwa srufi zalishi mofimu ina maana inayowakilishwa na mofu hivi kwamba mofimu ni dhana dhahania ambayo ni sehemu ya umilisi wa mtumiaji wa lugha husika kutokana na fasili hii mofimu ni lie maana iliyowakilishwa na mofu. Kwa misingi ya mantiki mofu ni sehemu halisi, hutamkika, huandikika na kuonekana ilhali maana mofimu ni dhahania na huwa imo akilini mwa mtumiaji wa lugha husika.
Lakini katika fasili ya Habwe na Karanja
(2004) wanaposema kuwa uhusiano kati ya mofu na mofimu ni ule wa umbo na yaliyomo au kiashiria na
kiashiriwa.
Kwa mfano,
1.
{a}+{na}+{pik}+{a}
Mofu {a-}
huwa na mofimu zifuatazo
a.
Mtenda
b.
Nafsi ya tatu umoja
c.
Kiambishi kipatanishi cha kisarufi cha ngeli ya kwanza
Kutokana na mfano huu mofu inaweza ikawa moja
lakini zikawa zaidi ya moja.
DHANA YA
ALOMOFU
Dhana ya alomofu.
Baada ya kueleza
dhana za mofu na mofimu tunaweza sasa kueoleza dhana ya alomofu. Richards et al
(1985) wanaeleza vizuri kuwa:
Alomofu ni umbo
mojawapo kati ya maumbo kadhaa tofauti yanayoiwakilisha mofimu moja.
Hartman (1970) naye anasema kuwa: Alomofu ni
umbo badala la mofimu fulani ambalo halibadili maana. Katika lugha ya
kiingreza, kwa mfano, kiambishi tamati /s/ cha wingi kina maumbo badala
yafuatayo:
a.
/s/
kama katika maneno cats, books, n.k.
b.
/z/
Kama katika maneno dogs, bags, n.k.
c.
/iz/
kama katika maneno classes, boxes, n.k
d.
/
Ɵ/ kama katika neno sheep.
Bauer (1983)
naye anasema kuwa: Alomofu ni mofu mojawapo katika seti ya mofu
zinazoiwakilisha mofimu fulani ambayo ina mazingira yake ya kifonetiki,
kileksika au kisintaksia (kisarufi).
Alomofu ni umbo
badala la mofimu fulani ambalo halibadili maana. Katika lugha ya kiingreza, kwa
mfano, kiambishi tamati /s/ cha wingi kina maumbo mbadala. Alomofu hufafanuliwa kama maumbo zaidi ya moja
(mbalimbali) ya mofimu moja.
Neno alomofu linatokana
na maneno mawili ambayo ni “alo” lenye maana ya zaidi ya moja au mbalimbali na
“mofu” lenye maana ya umbo.
Mfano
a.
M (u) +tu: wa+tu
b.
M (u) +ke: wa+ke
c.
Mw+alimu: w+alimu
d.
Mw+anajeshi: w+anajeshi
Katika mifano hiyo //mu// ya umoja ina maumbo mawili ambayo
ni //m// na //mw// halikadhalika //wa// ya wingi nayo ina maumbo mawili
ambayo ni //wa// na //w// hivyo maumbo haya yanaweza kuelezwa
kwa kanuni ifuatayo:
//mu//------->[m]/-k
------->[mw]/-I
//wa//-------->[wa]/-k
------->[w]/-I
Fasili tatu
tulizozitoa hapo juu zinaeleza sifa muhimu zinazoifafanua alomofu. Sifa hizo
niL
Alomofu ni umbo
Kama ilivyo kwa
mofu, alomofu ni umbo halisi ambalo ni sehemu neno fulani na ambalo hutamkwa na
kuandikwa. kwa hiyo alomofu ni mofu na sifa tuizozitoa kuhusu mofu ndizo
zinazofaa pia kuelezea alomofu.
Alomofu ni mofu mojawapo miongoni mwa mofu za mofimu
moja
Tofauti iliyopo
kati ya mofu na alomofu ni ndogo sana. Tofauti hiyo ni kuwa mofu huwa ni mofu
wakati ambapo umbo moja tu hutumika kuiwakilisha mofimu fulani. Aghalabu mofu
ambazo ni mizizi ya maneno, au tuseme mofu za kileksika huwa na umbo (mofu)
moja tu ambalo huwakilisha kitu fulani na mofu hizo huendelea kuitwa mofu za
momifu fulani kwani zina sura moja tu. popote zinapotokea hutokea na sura hiyo
hiyo na hazibadiliki. tutoe mfano wa mofu (imb). (imb) hubakia tu mahali popote
inapotokea kama:
a.
Imb+ a
(imba)
b.
si+imb+i
(siimbi)
c.
u+si+imb+e (usiimbe)
d.
tu+ta+
imb+a (tutaimba), n.k.
Wakati mofimu
fulani inapokuwa na umbo moja tu linaloiwakilisha mofimu hiyo, umbo hilo moja
huitwa mofu. Lakini, wakati mwingine mofimu moja huweza kuwakilishwa na mofu
(maumbo) kadhaa. katika hali kama hii mofimu inakuwa ni moja lakini maumbo
(mofimu yanayoiwakilisha mofimu hiyo yanakuwa mengi basi kila mofu miongoni mwa
mofu hizo kadhaa za mofimu moja itaitwa alomofu badala ya kuitwa mofu. Hii
inatuonysha au kutumumbusha kuwa hili ni umbo mojawapo mofu huwa hazina
mazingira (contex free), yaani kila mahali zinapotokea huitokea na umbo hilo
hilo, alomofu kwa upande wake zinatokea katika mazingira maalumu. kwa maneno mengine
alomofu zimegawana mahali pa kutokea, yaani mgawanyo wa kiutoano (complementary
distribution) hasa kwenye mipaka ya mofu hizo kiasi kwamba umbo la awali la
mofu ya kuathiriana tuliite umbo la ndani,
huwa ni tofauti na lile umbo linlotokea baada ya kuathiriana tuliite
umbo la nje. Tunaona, kwa mfano katika lugha ya Kiswahili wakati mwingine
maumbo ya ndani nay a nje ya mofu huwa tofauti,
Kwa mfano
Umbo la ndani Umbo la nje
a.
{lind} (linda) {linz}
(mlinzi)
b.
{chek}
(cheka) {chesh}
(mcheshi)
c.
{Pend}
(penda) {penz} (mpenzi)
d.
{u}+{ema} (wema )
e.
{pik}
(pika) {pish} (mapishi)
f.
{ing}
(mu+igo) {mw} (mwigo)
g.
{ma}
ma+ingi) {me} (mengi)
h.
{vi}
(v+ote) {vy} (vyote)
Wataalamu wa
mofolojia ya kiingereza, kwa mfano, wanaweza kueleza ni katika maneno yapi
mofu/s/ ya wingi itatumika na ni wapi mofu/z/ itatumika. Watakueleza, kwa
mfano, kuwa mofu/s/ hutumika katika maneno yanaoiishia na obstruenti hafifu
(voiceless obstruents) mofu /iz/ hutumika aktika maneno yanayoishia na
konsonanti vifyonzo (sabilanti consonants) kama /s, z, dz/. Na mofu /z/
hutumika katika sehemu zingine zote zilizosalia la muhimu tunalosema hapa ni
kuwa kiila alomofu ina mazingira yake ya kifonetiki, kileksika na kisintaksia.
Alomofu hazitumiwi ovyo ovyo tu.
MAZINGIRA
YA UTOKEAJI WA ALOMOFU
Alomofu hutokea katika mazingira maalumu. Mazingira mengine
yanatabirika na mengine hayatabiriki. Hata hivyo, alomofu huweza kutokea katika
mazingira ya aina tatu ambayo ni:,
·
Mazingira ya kifonolojia
·
Mazingira ya kileksika (kikamusi)
·
Mazingira ya kisarufi
Mazingira ya kifonolojia
Mazingira ya kifonolojia ya utokeaji wa alomofu hujitokeza
pale ambapo maumbo fulani hutokea kama alomofu kutokana na athari za
kifonolojia.
Mfano
M [u]/ -k
Mifano hiyo inaonesha jinsi umbo moja linavyoweza kubadilika
na kuwa katika muonekano tofauti huku maumbo yote hayo yakiendelea kubeba
taarifa ileile. Mabadiliko haya huwa yamesababishwa na athari za kifonolojia za
sauti fulani.
Umbo “mu” linatokea kama //mu// au //m//
linapofuatwa na konsonanti na linakuwa umbo //mw// linapofuatwa na
irabu.
Vilevile umbo //wa// linalojitokeza kama //wa// linapofuatwa
na konsonanti na linakuwa //w// linapofuatwa na irabu.
Vilevile mazingira ya kifonolojia hujidhihirisha katika
utendaji. Utokeaji wa alomofu za kauli huwa katika mazingira yanayotabirika na
yasiyotabirika.
Mazingira
yanayotabirika ya utendea
Mfano:1
a.
Funga – fung+i+a
b.
Lima – lim+i+a {- i-}
c.
Paka – pak+i+a
Mofu ya utendea {-i-} hutokea iwapo mzizi umebeba irabu
a, i, u.
//utenda//------->{- i-}/- mzizi [ a, i, u]
Mfano:2
a.
tema - tem+e+a
b.
soma - som+e+a {-e-}
c.
c) enda - end+e+a
Mofu ya utendea {-e-} inatokea iwapo mzizi umebeba irabu e
au o
//utendea//-------->{-
e-}/- mzizi [e, o]
Mfano:3
a.
Chukua - chuku+li+a
b.
Kimbia - kimbi+li+a {- li-}
c.
Pakua - pak+u+li+a
Mofu ya utendea {-li-} hutokea iwapo mzizi una irabu a, i,
u.
//utendea//-------->{-li-}/- mzizi mf I [a, i, u]
Mfano:4
a.
Zoa - zo+le+a
b.
Toa - to+le+a
{-le-}
c.
Toboa – tobo+le+a
Mofimu ya utendea {-le-} inatokea iwapo mzizi una irabu e au
o.
//utendea//-------->{-le-}/- mzizi mf I [e, o]
Mazingira ya utokeaji wa alomofu
ya utendeshi.
Mazingira yasiyotabiriki. Mfano
a)
lala-laza
b)
shuka-shusha
c)
lewa-levya
d)
ogopa-ogofya
e)
gawana-gawanya
Alomofu za utendeshi ni z, sh, vy, fy, ny.
Mazingira ya kileksika
Utokeaji wa alomofu katika mazingira ya kileksika huwa
tunazingatia ngeli za nomino kupitia mofu za umoja na wingi za nomino husika.
Mfano
a)
Kijana vijana
b)
Mtume mitume
c)
θRaisi maraisi
d)
θMungu θMungu
Katika mifano hiyo;
Alomofu za umoja ni ki, m, θ
Alomofu za wingi ni, vi, mi, ma, θ
//umoja//---->
ki /-konsonanti
//wingi//---->
vi/-k
//umoja//----->{m}/-k
//wingi//
---->{mi}/-k
//umoja//----> { θ}/-raisi
//wingi//----->{
ma}/-raisi
//umoja//----->{
θ}/-Mungu
//wingi//------>{
θ}/-Mungu.
Mazingira ya kisarufi
Mfano
a)
anapika - hapiki
b)
alipika - hakupika
c)
atapika - hakupika
d)
amepika - hajapika
a.
Alomofu za njeo ni:-na, li, ta, me,
i, ku, ja
b.
Alomofu za njeo uyakinishi ni; na,
li, ni, ta, me
c.
Alomofu za njeo ukanushi ni; i, ku,
ta, ja
VIGHAIRI
Vighairi ni dhanna inayohusu alomofu ambazo utokeaji wake
haufungamani na kanuni wala masharti yoyote.
Mifano
(a)
ki+tabu - vi+tabu
(b)
ki+jiko - vi+jiki
(c)
ki+nu - vi+nu
(d)
ch+umba - vy+umba
(e)
ch+eti - vy+eti
(f)
ki+oo - vi+oo
(g)
ch+oo - vy+oo
(h)
ch+umba - vy+umba
Mifano hiyo //ki// ya ngeli ya KI-VI umoja ina alomufu //ki-//
na //ch-// na mofu //vi-// ya wingi ina alomofu //vi// na //vy//.
ZINGATIA: Maneno choo, vyoo, chumba, vyumba, chetu, vyetu,
ni vighairi kwa sababu yanashiriki ngeli ya KI-VI lakini hayakubali mofu //ki-//
na //vi-// kukaa mwanzoni. Kimsingi //ch-// na //vy-// zipo kwenye ngeli
ya KI-VI lakini mwanzoni zipo zilivyo yaani, ki-vi itatokea tu kwenye
kitenzi cha upatanisho wa kisarufi.
Mfano; choo kimejengwa
Vyoo vimejengwa
KUTENGANISHA
MOFU NA ALOMOFU
Lugha ya Kiswahili ni lugha ambishi hivyo ina maneno ambayo
huundwa kwa mwandamo wa kisafu wa mofimu. Mofu hizi hupachikwa kabla na baada
ya mzizi kwa mfuatano ulio bayana.
Mfano;
A
B
(a) Anasoma
a-na- som-a
(b) Apikiwe a-pik-iw-e
(c) Fungana
fung-an a
Utenganishaji wa mofu katika maneno hayo unaonekana ni
rahisi kwa kuwa miundo ya maneno hayo inafahamika.
Tunapotenganisha mofu za lugha tusiyoijua ni lazima tuwe na
miundo yenye ruwaza zinazolingana ili tuweze kufananisha maana na maumbo mapya
yanayoandamana na maana mapya.
Mfano;
(a)
alatambuka - atatembea
(b)
Mulatambuka - mtatembea
(c)
Balatambuka - watatembea
(d)
Mukatambuka – mlitembea
(e)
Balayajula - watatambaa
Ingawa lugha hii yawezekana hatuitambui bado tunaweza
kutenga mofu zake kwa urahisi kwa kuwa kuna ruwaza zinazofanana na zile za
lugha tunayoifahamu. Kutokana na data ya lugha ya hapo juu (kihaya) kuna mofu
zifuatazo.
Mofu za za:
i.
//nafsi//--------- {a} -3-umoja
--------
{mu} -2-wingi
------
{ba} -3-wingi
ii.
//njeo//----------- {la} -ijayo
-----------
{ka} -iliyopita
iii.
//mzizi//---------- tambuk -
-----------
yajul –
KANUNI ZA KUTENGANISHA MOFU
Kanuni ya
kwanza; zingatia maumbo yenye maana sawa. Maumbo hayo huweza kufanana au
kuhitilafiana kiumbo lakini hutokea katika mazingira yaleyale. Mfano;
a.
Atakupiga a-ta-ku-pig-a
b.
Atampiga a-ta-m-pig-a
c.
Alikupiga a-li-ku-pig-a
d.
Utanipiga u-ta-ni-pig-a
e.
Utatupiga u-ta-tu-pig-a
f.
Mlijipiga m-li-ji-pig-a
Mofu
Mofu
nafsi--------- {a}-3-umoja
---------
{u}-2-umoja
----------
{m}-2-wingi
----------
{tu}-1-wingi
Mofu
njeo ------------- (ta)-ijayo
-------------
{li}-iliyopita
--------------
{na}-iliyopo
Yambwa ----------------
(ku)-wewe
---------
{m}-yeye
----------
{ni}-mimi
-----------
{ji}-binafsi
Kanuni ya pili; Hapa kinachozingatiwa ni maumbo yenye maana moja
lakini yasiyo na umbo sawa la kimofolojia.
Mfano;
a.
Mtumwa watumwa
b.
Mvulana wavulana
c.
Mjakazi wajakazi
d.
Mwenzi
wenzi
e.
Mwanadamu wanadamu
Mofu
Mofu
za idadi
//umoja//---------{m}/-k
--------
{mw}/-i
//wingi//---------
{wa}/-k
----------
{w}/-I
Kanuni ya tatu; Kanuni hii inadai kuwa alomofu moja au zaidi zimo katika
mtawanyo mkamilishano ambapo moja ikitokea basi ya pili haitokei. Yambwa na
yambiwa haziwezi kutokea katika mazingira yale yale.
Mfano
a.
Baba alinimpigia mimi simu
b.
Sisi tuliwamuona nyinyi
c.
Yeye alimwakuta wao
-
(m) na (mu)
-
(wa) na (w)
Zimo
katika mtawanyo mkamilishano au mgawanyo wa kiutowano
Kanuni ya nne;
Umbo moja na zaidi huweza kuwa katika mpishano huru kama maumbo hayo yana maana
moja na yametokea katika mazingira yaleyale.
Mfano
a.
Ngombe badala ya ng’ombe
b.
Khabari badala ya habari
c.
Lafiki badala ya Rafiki
d. Ntoto badala ya motto
Kanuni ya tano; inadai kuwa maumbo yenye maana tofauti ni Mofimu na
maumbo tofauti yenye maana sawa ni alomofu.
MATATIZO YA KUTENGANISHA MOFU
1. Tatizo la kwanza ni
kukosekana kwa umbo dhahiri la mofu
Mfano:
a.
θ+chungwa: ma+chungwa
b.
θ+bega : ma+bega
c.
θ+jiwe : ma+we
d.
θ+shati : ma+shati
Katika mifano hiyo mofimu za umoja ni {θ} na za wingi
ni {ma}
2. Tatizo la pili ni
kukosekana maneno asilia yanayozalisha maneno unde.
Mfano:
a.
Fupi – fupika –fupisha
b.
Refu - refuka –refusha
c.
Kau – kauka – kausha
Mifano hiyo ina maneno asilia na maneno unde. Maneno (fupi
na refu) ni maneno asilia ya maneno unde fupisha na refusha. Lakini (kau) sio
neno asili la neno (kauka na kausha) kwa sababu neno hilo (kau) halikubaliki
kwa maneno ya namna hiyo
3. Tatizo la tatu: ni
ugumu wa kutenganisha mofu katika maneno mwambatano.
Mfano:
a.
Mwanajeshi
b.
Mu-ana-jeshi
c.
Mw-ana-jeshi
d.
Mw-an-a-jeshi
e.
Mw-anajeshi
Maneno mwambatano yanaundwa kwa mzizi zaidi ya mmoja hivyo
huwa ni vigumu kubaini mofimu ni zipi na mizizi ni ipi. Hivyo mfano (b) mpaka (e)
imekosewa katika kutenganisha mofu. Ni vigumu kutenganisha mofu katika maneno
ya mwambatano.
MAKUNDI YA
MANENO
Katika lugha
kuna aina mbalimbali za maneno ambazo zina taratibu zake ambazo zinafanya ziwe
wazi au zimefungwa hivyo tunaweza kupata makundi mawili.
Makundi ya wazi na Makundi yaliyofungwa. Aina ya
maneno katika lugha ambazo unaweza kuyaingiza maneno mapya bila kizuizi. Mfano; nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi nk.
Makundi yaliyofungwa Mfano; viunganishi kama vile “na,
lakini, walakini nk ni maneno ambayo hayaruhusu maneno mapya kuingia kwa namna
mbalimbali. Viingizi=Maneno yanayotangulia katika kuunda sentensi. Mfano; Yesu
na Maria. Uundaji wa maneno mapya unahusu ubadilishaji wa maneno kuunda maneno
mengine.
Mfano;
a. uchekeshaji
b. ucheshi
c. vichekesho
Vyote ni
nomino za aina moja. -Unaweza kupata
vivumishi kutokana na kivumishi, nomino, kitenzi nk. Unaweza kunyumbua maneno
ya aina mbalimbali, hapa tutaanza na unyambuzi wa vitenzi. Kitenzi ni maneno
yanayotoa taarifa juu ya tendo linalifanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu.
Imefafanuliwa kwa kutilia maanani kama/kwa namna linavyotumika katika sentensi.
AINA ZA VITENZI
i)
Kitenzi
kikuu mfano; Analala
ii)
Kitenzi
kisaidizi mfano; Alikuwa analala
iii)
Kitenzi
kishirikishi mfano; Huyu ni mtoto.
Msingi uliotumika katika kuunda aina za vitenzi ni wa
kisintaksia sio kimofolojia. Msingi wa kimofolojia wa uainishaji wa sentensi ni
kutazama umbo la kitenzi ambalo linaweza kupatikana katika kamusi.
Mfano; la-la
Kul-a-la
Kuj-a
Maumbo ya vitenzi. Mizizi yenye sauti au herufi mbili.
Mfano; Ol-a, On-a -Jumla ya maneno
Sauti tatu na herufi nne Mfano; Teng-a, Pang-a. Maumbo
ya vitenzi yenye sauti tatu na herufi sita Mfano; Shang-a, Chungu-a -Sauti sita
na herufi saba
Mfano; Tengam-a
Katika Kiswahili kiuna maneno yamekopwa kutoka katika
lugha nyingine mfano, rudi, adabu, hakiki nk
Maumbo hayo pia
hubeba maana fulani ambapo yanaweza kuwa na sifa mojawapo kati ya hizi mbili;
Sifa elekezi, huwa ndani ya mzizi. Kwa kawaida kitenzi
hicho huambatana na yambwa nyingine kwa lazima. Mfano; O na a, O- imeruhusu
kuandamana na yambwa.
Si elekezi- Ni
mizizi isiyolazimisha kitenzi kuambatana na kipashio kingine.
VIAMBISHI NYAMBUZI KATIKA LUGHA YA
KISWAHILI
a.
Kiambishi
kitendwa. Hiki huwakilishwa na kiambishi “{-w-}”
b.
Kiambishi
kitendeka. Huwa mna umbo la “{-ik-}”, “{-ek-}”
c.
Kiambishi
kitendeshi. Huwa na maumbo ya {-ish-},{- esh-}, {-iz-},{- ez-}
d.
Kiambishi
kitendea. Huwa na umbo la i/e, {-il- }/{-el-}
e.
Kiambishi
kibadilifu (reversive). Huwa na umbo la{- o-}/{-u-}
f.
Kiambishi
kifungamanishi (static). Huwa na umbo la am
g.
Kiambishi
kishikanishi (contactive). Huwa na umbo la al
h.
Kiambishi
kitenganishi (resprocal). Huwa na umbo la {–an-}
NB: Hivi ni viambishi tofauti na viambishi vingine tulivyoviona. Mfano;
Teng-a. {a} - ni kiambishi kuonyesha dhamira.
MUUNDO WA MANENO
Neno huundwa na viambishi mbalimbali. Mfano wa maneno kutoka lugha ya
Kiswahili itatolewa mfano; vitenzi, nomino na vivumishi.
I. NOMINO
Nomino ni neno linalotaja kitu kitu, kiumbe, hali, dhana na tendo kama vile
ua, mti, tausi, mtandao,Ali, uzuri n.k. katika Kiswahili Nomino zina maumbo ya
aina nne:
a.
Umbo huru kama
vile; Simba, Jeni, Mombasa, baba n.k
b.
Umbo la kiambishi
awali na Mzizi kama vile m-zimu ambapo m-ni kiambishi awali na –zimu ni mizi wa
neno. Mifano mingine ya aina hiyo ni: mt-tu, ki-kapu, m-sumari, u-zuri, ji-ko,
ma-yai n.k
c.
Umbo la Kiambishi
awali, Kiambishi tamati na Mzizi, kama vile; ma-vun-o, m-chez-aji.
d.
Umbo la Mzizi na
Kiambishi tamati, kama: tuz-o,fund-i.
Katika Kiswahili, kama ilivyo katika lugha za familia ya Kibantu, nomino
hujigawa katika makundi yaitwayo ‘ngeli’ kisarufi. Kila nomino ya Kiswahili
maskani au makazi yake ni katika ngeli yake. Ngeli ni mgawanyo wa aina
mbalimbali za nomino, zaidi kwa msingi wa viambishi awali katika maumbo ya
nomino au vilevile kwa msingi wa viambishi vinavyotangulia maneno
yanayoambatana na nomino katika sentensi. Viambishi hivi kwenye maneno
yanayoambana na nomino katika sentensi hujulikana pia kama “viambishi vya
upatanisho wa kisarufi”. Kwa mfano tukio la kukutanisha nomino na kiwakilishi
kionyeshi huonyesha waziwazi asili ya nomino kwa kiambishi kama ifuatavyo:
a.
Mtoto huyu
b.
Kikapu hiki
c.
Yai hili
d.
Ubao huu
e.
Mti huu
f.
Nyumba hii
g.
Kucheza huku
h.
Longido hapa
Katika nomino hapo juu (a)-(h) zinaonesha kila moja kupatanishwa kwa
kiambishi kilichochorewa kistari pale kinapoambana na kiwakilishi kionnyeshi.
Hivi, kundi mojawapo la viambishi vya upatanisho wa kisarufi vya ngeli za
nomino katika Kiswahili.
Aidha, kuna matumizi ya nomino na upatanisho wa kisarufi yanayotokana na
athari za mifumo ya ngeli ya lugha nyingine za Kibantu kama ifuatavyo:
2. Katoto haka.
II. KITENZI
Kitenzi ni aina ya maneno inayoeleza tendo linalofanywa na nomino (Khamis,
2009:13). Mifano ya vitenzi ni kama vile og-a,
li-a, koho-a, sinzi-a, pumu-a n.k. anafafanua kwamba maumbo ya vitenzi
kuhusisha mzizi na kiambishi tamati –a ndiyo maumbo asili na ya msingi
yanayopatika katika kamusi.
Kihore (2009:13) anaeleza kuwa kitenzi ni aina ya maneno inayota taarifa
juu ya tendo linalofanyika au linalotendwa na kiumbe au kitu. Mfano ya vitenzi
katika Kiswahili ni pik-a, tembe-a, andik-a, som-a, abudu, shukuru, ag-a n.k.
anakubaliana na maelezo yaliyotolewa na Khamis (2009) kwa kusema katika mifano
hiyo hapo juu kuna vitenzi ambavyo vimeambikwa kiambishi mwishoni na vile
ambavyo havijaambikwa. Anasema; kwa kawaida, vitenzi vile vilivyoambikwa ni vya
asili ya lugha wakati vile ambavyo
havikuambikwa ni vya asili ya lugha ya kigeni.
Kutokana na maelezo hayo ya Kihore na Khamis (washatajwa), Wesana-Chomi
(2013:37) anahitimisha kwa kusema, Mofolojia ya kitenzi katika Kiswahili ni
muundo wa Mzizi tenzi pamoja na kiambishi tamati kimoja au zaidi. {MZ + K}.
Anatoa mifano ifuatayo:
2. Mzizi Kiambishi 3. Mzizi Kiambishi Kiambishi
·
Pig a pig an a
·
Som a som esh a
·
Let a let e a
·
Chuku a chuku liw a
·
Jeng a jeng ek a
Mifano katika (2) ni vitenzi vya msingi. Kitenzi cha msingi ni muundo wa
mzizi tenzi na kiambishi tamati kimoja tu ambacho ni kiishilizi (ishilizi).
Mara nyingi kiambishi tamati hiki huwa ni irabu “a”. Mifano katika (3) ni
vitenzi vya mnyumbuliko.
Anabainisha zaidi kuwa katika kitenzi cha msingi au kitenzi mnyambuliko
huongezwa kiambishi awali kimoja au zaidi na kuunda tungo kama vile:
a.
anasomo a. alinisomesha
b.
wataimba b. nilimsomea
c.
tumecheza c. ilisomwa
d.
hakusoma d. walituimbia
e.
hawataimba e. hauimbiki
f.
sijacheza f. aliimbisha
Chanzo: (Chomi, 2013:37)
Katika mifano hiyo, vitenzi hivyo si vitenzi tu bali ni tungo tenzi zenye
sifa za kisentensi. Vitenzi hivyo vimebeba viambishi vipatanishi kama vile; a,
wa, tu, ni, i, ye- ambavyo vinasababisha tungo tenzi hiyo kuwa na hadhi ya
sentensi. Kwa mfano Kihore (2009:14) anasema uambishaji wa viambsihi katika
mzizi wa kitenzi huto tungo ambazo ni sentensi kamili kwa kuwa vinahusisha
mtendaji wa tendo, wakati tendo lilipotendwa na anayetendewa tendo. Anabainisha
vitenzi vyenye sifa ya kuwa sentensi kamili kulingana na uambishaji kama
ifuatavyo:
a.
Nilimwona ni-li-mw-on-a
b.
Kimeanguka ki-me-anguk-a
c.
tunalala tu-na-lal-a
d.
wanasafiri wa-na-safiri
e.
tuliowaita tu-li-o-wa-it-a
f.
hawataondoka ha-wa-ta-ondok-a
g.
sijawatazama si-ja-wa-tazam-a
Swali. Vitenzi vya
lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za Kibantu vina sifa ya kuwa sentensi kama
sentensi nyingi. Jadili kauli hii.
Miundo ya vitenzi vya Kiswahili
i. Umbo la Mzizi na Kiambishi tamati
ishilizi
Kama ilivyoelezwa hapo juu hili ndiyo umbo msingi la vitenzi vya lugha ya
Kiswahili. Kwa mfano; som-a, lim-a, to-a. nyw-a, ny-a, f-a, j-a n.k.
ii. Umbo la Mzizi na Viambishi
nyambulishi; Kama vile:
a.
Pig-a pig-an-a, pig-an-ish-a,
pig-an-ish-w-a, pig-an-ish-i-w-a
b.
Fung-a fung-ish-a, fung-ish-an-a,
fung-ish-an-ish-a, fung-ish-an-ish-ik-a
Kihore (2009:14) anabainisha kuwa katika kiswahili umbo hili la kitenzi
linaweza kuruhusu mfuatano viamshi mpaka vinne (04) kama mifano hiyo
inavyoonesha.
iii. Umbo la Kitenzi ni
Umbo hili hujitokeza tu kwenye tunog yakinishi za njeo ya wakati uliopo
huwa pia haiandamni na viambishi katika tungo kama ilivyo kwa aina nyingine
iliyotangulia. Ni aina ya vitenzi ambavyo hutaja hali ya mtu. Kwa mfano:
a.
Juma ni mwalimu
b.
Asha ni mrembo
III. KIVUMISHI
Kivumishi ni neno linachukuzana na nomino likieleza zaidi sifa yake. Mfano
wa vivumishi katika lugha ya Kiswahili ni kama vile; kubwa, tamu, chungu, safi,
chafu n.k
Umbo la Vivumishi
Kivumishi kina maumbo mawili ambayo ni:
1.
Umbo Huru; kama
vile dogo, pana, gumu, zuri n.k
2.
Umbo
lililonyambulishwa; kama vile: nyenyeke-vu (nyenyekea), stahimili-vu
(stahimili) n.k. vivumishi vyenye umbo lililonyambulishwa ni vile vilivyotokana
na aina nyingine ya maneno.
Kwa kawaida katika tungo, vivumishi hasa vya asili ya lugha ya Kiswahili
huwa vinaambishwa viambishi vya nomino vinavyoandamana nazo. Kwa mfano:
a.
Mbuyu m-kubwa
b.
Mibuyu mi-kubwa
c.
Kikapu ki-dogo
d.
Mhogo m-chungu
Viambishi hivi hujulikana kama viambishi vya upatanisho wa kisarufi. Kwa
kawaida viambishi vya upatanishi huwa haviambishwa kwa vivumisho vilivyokopwa
kutoka lugha nyingine kama mifano ifuatayo inavyoonesha:
a.
Watu sita na siyo
(watu wasita*)
b.
Vikombe saba siyo
(vikombe visaba*)
c.
Mfuko laini siyo
(mfuko mlaini*)
d.
Msichana jamili
siyo (msichana mjamili*)
Katika mifano hiyo nomino zinazojitokeza mwanzoni mwa tungo hufuatwa na
vivumishi ambavyo vimekopwa kutoka lugha ya Kiarabu.
IV. KIELEZI
Ni aina ya maneno yanayoeleza zaidi kuhusu kitenzi kinachoambatana nacho
katika tungo. Mfano wa vielezi katika Kiswahili ni vizuri, polepole, sana, mno
n.k.
Maumbo ya Vielezi
Kimofolojia vielezi hugawanyika katika makundi matatu
1.
Kundi la umbo huru
(Vielezi Halisi) k.m sana, mno, upesi, harka n.k
2.
Kundi la umbo
lilioambikwa (Vielezi Ambikwa) kama vile vi-zuri, vye-ma, ki-dogo n.k
3.
Kundi la Umbo
radidi kama vile; kimyakimya, polepole, chinichini n.k
Katika tungo, vielezi huwa haviambishwi viambishi vya upatanishi wa
kisarufi kama ilivyo kuhusiana na vivumishi vilivyojadiliwa hapo juu. Aidha,
katika tungo vielezi tofauti huweza kuandamana na kitenzi kama mfano ufuatao
unavyoonesha:
a.
Anatembea haraka
sana
b.
Tumekula vizuri
kabisa
c.
Wanaongea polepole
mno
d.
Mmeshindwa vibaya
kweli kweli
Swadakta
ReplyDeleteKazi njema, kazi murua
ReplyDeleteMarejeleo mbona hayapo ambatanisha mheshimiwa
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteKazi murua...kongole
ReplyDeleteIpo viziri
ReplyDeleteKazi nzuri ... Naomba ueleze uamilifu wa mofu
ReplyDeleteMAREJEREO SIYAONI
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDelete